WAZIRI wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof Adolf Mkenda,akizungumza na waandishi wa habari leo Aprili 11,2023 jijini Dodoma kuhusu kutoa ruhusa ya wanafunzi 337 waliofutiwa matokeo kidato cha nne kurudia mitihani Mei 2,mwaka huu.
Na.Alex Sonna-DODOMA
WIZARA ya Elimu,Sayansi na Teknolojia imewaruhusu wanafunzi 337 waliofutiwa matokeo ya kidato cha nne kutokana na kufanya udanganyifu na kuandika matus kurudia tena mitihani hiyo Mei 2 mwaka huu.
Hayo yameelezwa leo Aprili 11,2023 jijini Dodoma na Waziri wa Wizara hiyo,Prof Adolf Mkenda wakati akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dodoma ambapo amesema wamejadiliana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA) ili kuona namna ya wanafunzi hao kufanya mtihani mapema kabla ya duru nyingine na suala hilo halitarudiwa tena.
“Nimeelekeza wanafunzi hao kama wakitaka wawasiliane na Baraza ili kufanya mtihani wa kidato cha nne na utatolewa wakati wa mtihani wa kidato cha sita ambao utaanza Mei 2 hadi 22, mwaka huu,”alisema.
Amesema matokeo yalivyotoka Baraza la Mitihani (NECTA) liliwafutia watahiniwa 337 wa kidato cha nne ambapo kati ya hao wanafunzi 333 walifutiwa kutokana na sababu ya udanganyifu na wanawafunzi wanne sababu ya kuandika matusi kwenye karatasi za majibu.
Amebainisha kuwa shule zilizofanya udanganyifu ambazo ni Twibhoki, Thaqaafa, shule ya Mnemonic Academy ya Zanzibar na Cornel zitaendelea kuwa chini ya uangalizi na serikali haiwezi kukubali kusajili shule kwenda kuwa kiwanda cha kuharibu mfumo wa elimu.
“Kati ya wanafunzi 333 ambao matokeo yao yalizuiliwa wanafunzi 206 wanatoka katika shule mbili tu ambazo ni Twibhoki mkoani Mara na Thaqaafa jijini Mwanza, takribani mbili ya tatu ya wanafunzi wote waliozuiliwa matokeo wanatoka katika shule hizi mbili,”alisema.
“Kwa kawaida matokeo yanapofungiwa watahiniwa sababu kama hizo wanawez kuomba kufanya tena mtihani katika duru inayofuata kama watahiniwa binafsi,”amesema Prof. Mkenda.
Amesema kwa sababu hiyo wamefanya mazungumzo na Baraza la Mitihani ili kuona jinsi ambavyo wanafunzi hao wataweza kurudia kufanya mitihani kuanzia Mei 2 mwaka huu pamoja na wanafunzi wa kidato cha sita.
Aidha amesema kuwa gharama za uendeshaji wa mtihani huo zitakuwa ndogo na kama ingeendeshwa nje ya utaratibu huo ingegharimu serikali zaidi ya Sh.Bilioni moja.
“Wasimamizi wa mitihani watakuwa wale wale wa kidato cha sita na watafanya kwa utaratibu utakaowekwa na utafungwa kwenda kusahihishwa.Hii ni mara ya mwisho kufanya hivi hatuwezi kuingiza nchi kwenye gharama hizi,”amesema Prof.Mkenda
“Naamini itakuwa mara ya mwisho nataka wazazi wajue wala hailipi kushinikiza udanganyifu na watu wapewe fedha waliohusika kuwadanganya watoto wetu walaaniwe,”amesema Prof.Mkenda
Waziri Mkenda amesema wizi wa mihani una madhara makubwa kwani hawawatendei haki watahiniwa ambao hawajaoneshwa mitihani.
“Nasema hivi ili wazazi walimu na watanzania tuwe imara kukemea jambo hili na tuwe shupavu kupambana bila kulegalega.Ni suala la haki kuhakikisha watahiniwa wote wanafanya mitihani katika mazingira sawa hakuna ambaye anaruhusiwa kuona mtihani au kuingia na majibu,”amesema .
Amesema wizi wa mtihani unafundisha vijana wizi na utovu wa maadili kwani kwa sasa watu wengi wanazungumzia suala la malezi na maadili kushuka,
“Fikiria unaenda kutibiwa na Dakatari ambaye amepita kwa kuoneshwa mitihani una uhakika kweli utahudumiwa vizuri au rubani ambaye hakufaulu kwa haki, tutakapoanza kuruhusu tutakuwa tunaharibu mfumo wa elimu,”amesema
Prof Mkenda amesema kufutiwa kwa matokeo kwa vijana hao ni jambo ambalo linatia uchungu na hawafurahii watoto kukaa nyumbani hasa mabinti.
“Kinachoumia katika wanafunzi hao 2.3 wanatoka katika shule ambazo zilikuwa zimewekwa katika mfumo wa udanganyifu wapende wasipende,aliyekataa alichapwa na mwalimu
“Kuna shule mmiliki wa shule alilipa askari,kuna wanafunzi wengi wameingia katika mkumbo kunakuwa na tamaaa ya kufanya vizuri wanakuwa na uwezo lakini wameingia katika mkumbo,”amesema wa
Amesema shule ambazo zinazoonekana kufanya udanganyifu wanaziweka chini ya uangalizi kwani hawawezi kukubali kusajili shule ambazo ni kiwanda cha udanganyifu na kuharibu mfumo wa elimu.
Amesema wapo tayari kufuta shule ambazo zitahusika katika udanganyifu na mtihani wa kidato cha sita unaotarajiwa kuanza Mei 2 mwaka huu.
“Wale wanaopanga kufanya udanganyifu naomba niwaambie hatutaki udangayifu ipo shule moja wanafunzi wamepewa wafanye mtihani wale wa juu ya darasa,Shule ambazo zimehusika natuma salama kwa wazazi mna taarifa shule zipo chini ya uangalizi kwanini umepeleke mwanao kwani shule ni hizo tu,”amesema
Amesema kesi zipo mahakamani za watu waliohusika na wizi wa mtihani ambapo amedai wanazifuatilia na mashtaka yanaendeshwa vizuri ili stahiki zichukuliwe.
“Wale wote waliohusika wachukuliwe hatua kwa sabahu hawa wangefanya kazi zao vizuri sisi tusingekuwa na kazi tena ya kuokoa vijana wetu,”amesema
Hata hivyo Prof Mkenda ameziagiza kamati za mitihani za mikoa kuongeza umakini hasa Mwanza Mara na Shinyanga ijipange vizuri kuhakikisha makosa hayo hayajitokezi tena.
Social Plugin