******************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KLABU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na alama tatu mbele ya Kagera Sugar na kujikita zaidi kileleni mara baada ya kushinda mabao 5-0, mchezo ambao ulipigwa kwenye dimba la Azam Complex Jijini Dar es Salaam.
Yanga Sc ilianza kupata bao kupitia kwa Aziz Ki kwa mkwaju wa penati baada ya Fiston Kalala Mayele kuchezewa rafu ndani ya kumi na nane.
Aziz Ki aliendelea kuwanyoosha mabeki wa upinzani kwani alifanikiwa kupachika bao la pili kwa shuti kali ambalo lilimshinda kipa na kuingia moja kwa moja wavuni na baadae aliweza kupachika bao lake la tatu kwenye mchezo huo Hat Trick.
Bao la tatu limefungwa na Fiston Mayele ambaye alifunga kipindi cha pili na kuweza kupumzika kwenye mchezo huo, bao hilo la Mayele linamfanya aendelee kukaa kileleni kwa wapachikaji wa mabao akiwa na mabao 16 kwenye ligi.
Benard Morrison aliingia kipindi cha pili na kuweza kuisaidia timu yake kupata bao la nne kwenye mcehzo huo kwa kupiga shuti kali ambalo lilizama moja kwa moja wavuni na baadae bao la tano likifungwa na Azizi Ki kwa mkwaju wa penati.
Social Plugin