Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SHINYANGA WAADHIMISHA MIAKA 59 YA MUUNGANO WA TANGANYIKA NA ZANZIBAR, RC MNDEME AFUNGUA ZAHANATI YA MASEKELO

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zimamoto Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA  

MKOA wa Shinyanga umeadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, pamoja na kuifungua Rasmi Zahanati ya Masekelo.

Maadhimisho hayo yamefanyika leo April 26,2023 katika viwanja vya Zima Moto vilivyopo maeneo ya nguzo nane, pamoja na kwenda kuzindua Zahanati ya Masekelo iliyopo Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, akizungumza kwenye maadhimisho hayo ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, amewataka wananchi kuuenzi Muungano kwa kudumisha Amani, upendo na mshikamano.

Amesema ili kuwaenzi waasisi wa Muungano hayati Shekhe Abeid Amani Karume Rais wa kwanza wa Zanzibar, na Rais wa Tanganyika kwa wakati huo hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ni kuendelea kudumisha Amani.

"Muungano wetu umetuletea undugu, uzalendo, Amani, mshikamano na utulivu, hivyo ni vyema tukaendelea kuuenzi kwa kudumisha amani, upendo na mshikamano," amesema Mndeme.

Aidha, amesema ndani ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mkoa wa Shinyanga umepiga hatua kubwa kimaendeleo ikiwamo Sekta ya Afya, Elimu, Maji, Nishati ya umeme pamoja na ujenzi wa miundombuni ya barabara.

Amesema kabla ya Muungano Mkoa wa Shinyanga ulikuwa na Zahanati 10, lakini baada ya Muungano hadi mwaka (2023) zimefika Zahanati 250, vituo vya afya kutoka Sifuri hadi 46 na Hospitali kutoka moja hadi 10.

"Ninafurahi kuadhimisha miaka 59 ya Muungano pamoja na kufungua Rasmi Zahanati ya Masekelo ambayo itahudumia wananchi wapatao 19,332 nawaomba akina mama muitumie vizuri kupata huduma ya afya ya uzazi na mhudhurie Kliniki kwa wakati ili mjifunge salama," amesema Mndeme.

Naye Mtendaji wa Kata ya Masekelo Revina Nyagawa, amesema ujenzi wa Zahanati hiyo ya Masekelo ulianza mwaka 2015, na umeshagharimu kiasi cha fedha Sh. Milioni 104.7.

Nao baadhi ya viongozi wakitoa salamu, wamewasihi Watanzania kujivunia Muungano na kuendelea kudumisha Amani, upendo na mshikamano.

Kauli mbiu katika maadhimisho hayo ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar Umoja, Mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zimamoto Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zimamoto Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zimamoto Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.

Mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zimamoto Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.
 Mkuu wa wilaya ya Kahama Mboni Mhita akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zimamoto Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zimamoto Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.
Katibu Tawala wa wilaya ya Shinyanga Boniphace Chambi akizungumza kwenye Maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mkoani Shinyanga.
 Mbunge wa Jimbo la Ushetu Emmanuel Cherehani akizungumza kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yaliyofanyika kimkoa katika viwanja vya Zimamoto Nguzo nane Manispaa ya Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, (kushoto) akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya kufungua Rasmi Zahanati ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga., (kulia) ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme, (kushoto) akiweka jiwe la msingi kwa ajili ya kufungua Rasmi Zahanati ya Masekelo Manispaa ya Shinyanga (kulia) ni Meya wa Manispaa ya Shinyanga Elias Masumbuko.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akipanda Mti katika Zahanati ya Masekelo.
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi akipanda Mti katika Zahanati ya Masekelo.
Katibu wa CCM Mkoa wa Shinyanga Donald Magesa akipanda Mti katika Zahanati ya Masekelo.
Viongozi wakiwa meza kuu kwenye maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mkoani Shinyanga.
Maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yakiendelea mkoani Shinyanga.

Maadhimisho ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yakiendelea mkoani Shinyanga

Awali Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) akisalimiana na viongozi mbalimbali alipowasili kwenye viwanja ya Zimamoto Nguzo Nane kwa ajili ya kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mkoani humo.
Viongozi wakitoa salamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme alipowasili kwenye viwanja vya Zimamoto Nguzo Nane kwa ajili ya kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mkoani humo. 
Viongozi wakitoa salamu kwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (kushoto) alipowasili kwenye viwanja vya Zimamoto Nguzo Nane kwa ajili ya kuadhimisha miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mkoani humo. 
Viongozi wakipiga picha ya pamoja.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com