Wananchi wa Kijiji cha Itete wilayani Malinyi mkoani Morogoro imewalazimu kupiga kura kuwabaini wafugaji wakorofi ambao wamekuwa wakisababisha migogoro katika kijiji hicho.
Ililazimika kupiga kura ya Siri ya maandishi kuwataja wafugaji hao ili Mamlaka za serikali ziweze kuwashughulikia.
Mkuu wa Wilaya ya Malinyi Sebastian Waryuba na kamati ya Usalama Wilayani humo walilazimika kufika katika kijiji hicho ili kumaliza changamoto ya wafugaji kulishia Mifugo katika mashamba ya wakulima ambayo yapo katika skimu ya umwagiliaji.
Kufuatia maoni ambayo aliyapokea katika mkutano wa hadhara Kijiji cha Itete Waryuba alilazimika kuwataka wananchi kupiga kura kutaja majina ya wafugaji wakorofi baada ya diwani wa Kata ya Itete Mheshimiwa Anatory Libawa kubainisha kuwa lipo kundi la wafugaji wakorofi ambao husababisha migogoro katika eneo hilo.
Na matokeo ya kura hizo zaidi ya wafugaji Kumi na Tano waliangukiwa na kura za wananchi ambapo mkuu wa wilaya ya Malinyi amewataka wafugaji hao pamoja na watendaji wao wa vijiji kuripoti ofisini kwake alhamisi Aprili13,2023 saa tano asubuhi.
Awali wananchi wa Kijiji hicho walilalamimikia wafugaji ambao waliingia kijijini miaka kumi iliyopita kuwa wanaharibu kilimo Cha umwagiliaji ambacho ni mpango wa serikali katika uzalishaji wa mazao.
Kulingana na matokeo hayo mkuu wa wilaya amepiga marufuku kuanzia kuanzia Sasa Mifugo kukaribia skimu ya umwagiliaji ya Itete ambayo imejengwa kwa zaidi ya shilingi bilioni 1 na serikali.
"Viongozi wa skimu simamieni hilo hilo na kuanzia Sasa nikisikia Mifugo katika skimu tutawajibishana na serikali ya Kijiji kuweni wabunifu tengenezeni mfumo mzuri wa ulinzi katika skimu"alisema.
Kwa mujibu wa takwimu zilizopo Kijiji cha Itete kilitakiwa kuwa na Mifugo yaani Ng'ombe so zaidi ya 1500 ambapo mpaka Sasa kwa mujibu wa wananchi kuna ongezeko kubwa la Mifugo.
Social Plugin