Milembe Selemani(43)
Milembe Selemani(43), mkazi wa mtaa wa Mseto halmashauri ya mji Geita, aliyekuwa kitengo cha ugavi mgodi wa GGML, ameuawa kwa kukatwa viungo vya mwili wake na watu wasiojulikana na mwili wake kutupwa kwenye moja ya nyumba alizokuwa anajenga zilizopo mtaa wa Mwatulole Kata ya Buhalahala.
Kaimu Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Geita Berthaneema Mlay, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku watu wanne wakishikiliwa kwa ajili ya uchunguzi.
Social Plugin