Meneja wa Shirika la Nyumba (NHC) Angelina Magazi (kushoto) akimkabidhi nyaraka mbalimbali ikiwemo ramani ya ujenzi wa jengo la kisasa la kibiashara linalojengwa katika eneo la kiwanja cha shirika hilo kilichopo eneo la uwekezaji la Bukondamoyo , Halmashauri ya Manispaa ya Kahama anyepokea ni Mhandisi Mburuga Matamwe na Mshauri wa mradi wa Shirika Godfrey Mkumbo na kulia anayeshuhudia ni mkandarasi Mhandisi Masumbuko Majaliwa na kushoto ni Msanifu wa mradi NHC ,Robert Kintu.
Mshauri wa mradi wa Shirika la Nyumba Tanzania ( NHC) Godfrey Mkumbo akiwaonesha eneo mradi wa ujenzi wa jengo la kisasa linalojengwa eneo la uwekezaji la Bukondamoyo , Halmashauri ya Manispaa ya Kahama , litakalokuwa na vyumba vya maduka vya kisasa, Migahawa, Super Market , sehemu ya kuosha magari , wengine ni meneja wa NHC mkoa wa Shinyanga , Angelina Magazi, meneja Mradi wa NHC , Mhandisi Mburuga Matamwe na Msanifu wa Mradi NHC ,Robert Kintu.
Msanifu wa Mradi wa NHC Robert Kintu wa katikati akiwaonesha maafisa wa NHC ramani ya ujenzi wa jengo la kisasa litakalokuwa na vyumba vya maduka 84 , Migahawa, Super Market na eneo la kuonsha magari ambalo linajengwa katika eneo la uwekezaji lililopo Bukondamoyo , Manispaa ya Kahama.
Meneja wa NHC wa mkoa wa Shinyanga , Angelina Magazi wa katikati akiongoza maafisa wa Shirika hilo katika mradi wa ujenzi jengo la kisasa litakalokuwa na vyumba vya kisasa vya maduka , migahawa , super market , sehemu za kuonya magari ambalo mradi huo umeanza kutekelezwa katika eneo lao la Bukondamoyo , Halmashauri ya Manispaa ya Kahama.
Msanifu wa Mradi wa NHC ,Robert Kintu wa ujenzi wa jengo la kisasa katika eneo la uwekezaji la Bukondamoyo katika Halmashauri ya Manispaa ya Kahama unaotekelezwa na shirika hilo ambalo jengo hilo litakuwa na vyumba vya kisasa vya maduka 84 , Super Market , Migahawa na sehemu ya kuonya magari akiwaonesha maafisa wa NHC ramani ya mradi huo ulioanza kutekelezwa wilayani Kahama
Na Patrick Mabula , Kahama .
Shirika la Nyumba Tanzania (NHC) limeanza kutekeleza mradi wa ujenzi wa jengo la kisasa katika eneo la uwekezaji lililopo Bukondamoyo katika Halamashauri ya Manispaa ya Kahama kwenye eneo lake ambako wanajenga vyumba vya kisasa vya maduka , migahawa, Super Market pamoja na sehemu ya kuoshea magari.
Akiongea katika eneo la mradi huo leo, Meneja wa Shirika la Nyumba wa Mkoa wa Shinyanga , Angelina Magazi amesema mradi huo umeanza kutekelezwa katika kiwanja cha shirika hilo kilichopo eneo la viwanda la Bukondamoyo maarufu kwa jina la Dodoma Manispaa ya Kahama.
Magazi amesema NHC katika mradi huo kutakuwa na vyumba vikubwa vya kisasa vya maduka vipatavyo 84, Migahawa, Super Market na sehemu ya kuosha magari na watapangisha kwa wateja watakao kidhi masharti kwa gharama nafuu kwa lengo la kusaidia ajira kwa watu.
Meneja Mradi wa Shirika la Nyumba Tanzania , Mhandisi Mburuga Matamwe amesema ujenzi wa mradi huo wa majengo ya kisasa ni uwekezaji mkubwa unategemea kugharimu kisasi cha zaidi ya shilingi bilioni moja na tayari mapema utekelezaji wake umeshaanza.
Mshauri wa mradi huo , Mhandisi Godfrey Mkumbo amesema ujenzi wa jengo hilo litakalokuwa na vyumba vikubwa vya maduka vya kisasa utekelezaji wake unatarajia kukamilika katika kipindi cha miezi sita ijayo na hiyo itakuwa ni fursa kwa watu kupangishwa kwa gharama nafuu.
Kwa upande wake mkandarasi wa mradi huo , Mhandisi Masumbuko Majaliwa amesema tayari ameanza utekelezaji wa maradi huo na kuahidi kukamilisha ndani ya kipindi atakachokuwa amepewa kadri ya mkataba unavyosema.
Naye Msanifu wa mradi huo Arch Robart Kintu amesema mradi huo upo eneo zuri lililopo karibu na stendi ndogo ya magari ya abiria ya Bukondamoyo , katika eneo la viwanda la Manispaa ya Kahama ambapo watu watapata fursa ya kujiajiri na pale utakapokamilika katika kipindi cha miezi sita na utachochea maendeleo katika manispaa ya Kahama.
Social Plugin