Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ASKOFU DK. NZELU ASIMIKWA KUWA ASKOFU WA KANISA LA KKKT DAYOSISI KUSINI MASHARIKI YA ZIWA VICTORIA

Askofu Dk. Yohana Nzelu akiwa ameshasimikwa kuwa Askofu wa Kanisa la (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayoundwa na Mikoa miwili ya Shinyanga na Simiyu.
Askofu Dk. Yohana Nzelu akisimikwa kuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayoundwa na Mikoa miwili ya Shinyanga na Simiyu, (kulia) Askof Dk. Fredric Shoo, (kushoto) ni Askofu Dk. Emmanuel Makala ambaye amestaafu.

Na Marco Maduhu, SHINYANGA

ASKOFU Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT)Dk. Fredric Shoo, amemsimika Rasmi Askofu Dk. Yohana Nzelu kuwa Askofu wa Kanisa la (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayoundwa na Mikoa miwili ya Shinyanga na Simiyu, sambamba na msaidizi wake Dk. Daniel Mono.

Tukio hilo la kumsimika Askofu Dk. Yohana Nzelu na msaidizi wake Dk. Daniel Mono, limefanyika leo Aprili 30, 2023 na kuhudhuriwa na waumini wa Kanisa hilo, na viongozi mbalimbali wa Serikali huku Mgeni Rasmi akiwa ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akimwakilisha Rais Samia.

Askofu Shoo akizungumza kwenye Ibada, ameitaka jamii kutenda mambo mema ambayo yanampendeza mwenyezi mungu, pamoja na kusimamia malezi na makuzi dhidi ya watoto ili wakue katika maadili mema.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme akimwakilisha Rais Samia, amesema Serikali ya awamu ya sita inatambua mchango mkubwa wa Taasisi za kidini hapa nchini ikiwamo kutoa huduma za kijamii na Kiroho pamoja na kudumisha Amani ya nchi.

Amesema Serikali ya awamu ya Sita itaendelea kushirikiana na viongozi wa kidini ili kuhakikisha wananchi wanaishi kwa Amani, utuluvi na upendo.

Katika hatua nyingine Mndeme, amewataka wananchi wa Mkoa huo kuacha kuiga mambo ya kigeni vikiwamo vitendo vya ushoga, usagaji bali waishi na kuzitii amri 10 za Mungu.

"Nimeanzisha kampeni ya usiniguse yaani 'Don't touch me kwa kuwafundisha watoto wasikubali kufanyiwa vitendo viovu bali watoe taarifa na viendo hivyo vikemewe kwa nguvu zote"amesema Mndeme.

Kwa upande wake Askofu Dk. Yohana Nzelu, amesema wataendelea kushirikiana na Serikali kwa kutoa huduma za kiroho kwa jamii pamoja na kueneza upendo na Amani.

'Mimi nitakuwa tayari kushirikiana na Serikali kwa Mikoa ya Shinyanga na Simiyu, na nina ipongeza Serikali ya awamu ya Sita kwa maendeleo wanayoyafanya, lakini naomba baadhi ya Barabara kama Old Shinyanga kwenda Solwa na Kahama kwenda Kakola ziboreshwe"amesema Askofu Nzelu.
Zoezi la kumsimika Askofu Dk. Yohana Nzelu kuwa Askofu wa Kanisa la (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayoundwa na Mikoa miwili ya Shinyanga na Simiyu likiendelea.
Zoezi la kumsimika Askofu Dk. Yohana Nzelu kuwa Askofu wa Kanisa la (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayoundwa na Mikoa miwili ya Shinyanga na Simiyu likiendelea.
ASkofu Dk. Yohana Nzelu akisimikwa kuwa Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) Dayosisi ya Kusini Mashariki ya Ziwa Victoria inayoundwa na Mikoa miwili ya Shinyanga na Simiyu, (kulia) Askof Dk. Fredric Shoo, (kushoto) ni Askofu Dk. Emmanuel Makala ambaye amestaafu.
Viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme (wapili kutoka kulia) akifuatiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga Johari Samizi na (kulia) ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Shinyanga Prof, Siza Tumbo wakiwa kwenye Ibada ya kusimikwa Askofu Dk.Yohana Nzelu na msaidizi wake Dk.Daniel Mono.
Waumini wa Kanisa la (KKKT) wakiwa kwenye Ibada ya kusimikwa Askofu Dk Yohana Nzelu na msaidizi wake Dk. Daniel Mono.
Maaskofu wakiwa kwenye hafla ya kusimikwa Askofu Dk. Yohana Nzelu na msaidizi wake Dk. Daniel Mono.
Maaskofu wakiwa kwenye hafla ya kusimikwa Askofu Dk. Yohana Nzelu na msaidizi wake Dk. Daniel Mono.
Maandamano yakiendelea katika hafla ya kusimikwa Askofu Dk. Yohana Nzelu na msaidizi wake Dk. Daniel Mono.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com