Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BODI YA MFUKO WA BARABARA YASHIRIKI MANESHO YA TEKNOLOJIA NA UBUNIFU

Kaimu Meneja wa Mfuko wa Barabara Eng. Rashid Kalimbaga, akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu Mfumo wa ufuatiliaji hali ya barabara unaotumiwa na wananchi katika kutoa taarifa za hali ya barabara, katika kilele cha maonesho ya Teknolojia na Ubunifu jijini Dodoma.
Meneja Msaidizi Utawala na Fedha CPA John Aswile, kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara (wa kwanza kushoto), akiwa kwenye banda la Bodi hiyo baada ya kutembelea maonesho ya Teknolojia na Ubunifu jijini Dodoma.
Bwana Comfort Mgalula kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara akigawa vipeperushi vinavyoelezea matumizi ya mfumo wa ufuatiliaji wa hali ya barabara (BARABARA APP) kwa baadhi ya watoto waliotembelea banda la la Bodi hiyo. Kwenye maonesho ya Teknolojia na Ubunifu jijini Dodoma. Wanaoshuhudia ni Agnes Agustine na Joseph Mwabulwa
Bw. Comfort Mgalula kutoka Bodi ya Mfuko wa Barabara akizungumza na Bw. Elibariki Eliud (wa kwanza kushoto) kuhusu utendaji kazi wa mfumo wa ufuatiliaji wa hali ya barabara unaotumiwa na wananchi kupitia simu ya kiganjani katika maonesho ya Teknolojia na Ubunifu jijini Dodoma

Picha na RFB

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com