Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

CHUO CHA TAIFA CHA UTALII (NCT) CHAFANYA MDAHALO KUADHIMISHA MIAKA 59 YA MUUNGANO




Kaimu Mkuu wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Florian Mtey akizungumza alipokuwa akitoa hotuba yake ya kufungua rasmi Mdahalo wa maadhimisho wa sherehe za miaka ya 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar uliofanyika katika Ukumbi wa mikutano wa Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.

Mkufunzi katika Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Naiman Mbise akizungumza alipokuwa akitoa mada iliyohusu kutengeneza Viwango ili kutoa Huduma bora katika Seka ya Utalii.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Idara ya Sayansi, Siasa na Utawala wa Umma, Dkt. Richard Mbunda akitoa mada iliyohusu Umoja na Mshikamano ndio nguzo ya kukuza uchumi wetu katika Sekta ya Utalii.

Kaimu Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Utalii (NCT), Taaluma, Tafiti, na Ushauri Bi. Jesca William akizungumza alipokuwa akitoa salamu za utangulizi na kuwatambulisha wageni mbalimbali waliohudhuria Mdahalo huo.
(PICHA NA: HUGHES DUGILO)

Na: Hughes Dugilo, DAR ES SALAAM

Kaimu Mkuu wa chuo cha Taifa cha Utalii (NCT) Dkt. Florian Mtey amesema katika kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha Sekta ya Utalii inaendelea kuchangia pato la Taifa, tayari chuo hicho kimeanza kutekeleza Programu mbalimbali ili kuendana na uhitaji wa soko la ajira nchini. Dkt Mteyi ametoa kauli hiyo Jijini Dar es salaam wakati wa Mdahalo wa maadhimisho wa sherehe za miaka ya 59 ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo amesema kwa mwaka 2022 pekee Sekta ya Utaii imefanikiwa kukusanya Dola za Kimarekani Bilioni 1.4. Amesema fedha hizo zimetokana na matunda ya Filamu ya ‘Tanzania – The Royal tour’ iliyozinduliwa na Rais wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan pamoja na mambo mengine, Watalii wameendelea kuongezeka kutoka Mataifa mbalimbali na kuongeza mchango wa Pato la Taifa (GDP). ”Tangu Rais Dkt Samia Suluhu Hassan azindue Filamu ya ‘The Royal Tour’ tumeona wawekezaji wengi wamemiminika katika mbuga zetu, haya ni matunda ya ile Filamu na sisi kama Chuo tunaendelea kuunga mkono jitihada hizi hasa kwa kushirikiaa na wadau pamoja na Sekta Binafsi” Amesema Dkt. Mtey. Kwa upande wake Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Idara ya Sayansi Siasa na Utawala wa Umma Dkt. RIchard Mbunda amesema muungano umeleta faida katika Sekta ya Utalii ikiwemo kurahisisha upatikanaji wa masoko hasa kwa wawekezaji wanaowekezaZanzibar na Tanzania Bara. ”Muungano huu umewasaidia sana wawekezaji hasa kweye upande wa masoko ndmana leo watalii wanaenda Zanzibar lakini wamefikia Dar es salaam au wengine wanaenda kutalii katika visiwa vya Zanzibar lakini wamefikia Dar es salaam” Amesema Dkt Mbunda. Itakumbukwa kuwa mwaka 2015 hadi 2020 Serikali ya Mapinduzi Zanzibar pamoja na Tanzania Bara zilifanya vikao takribani 85 kujadili kero mbalimbali za Muungano ambapo katika vikao hivyo kero 18 ziliibuliwa huku kero 11 zikipatiwa ufumbuzi.
PICHA MBALIMBALI ZA WASHIRIKI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com