Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeendesha zoezi la upandaji miti katika maeneo ya hifadhi za miundombinu ya maji ikiwa ni utekelezaji wa agizo la Waziri Mkuu Wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania la kupanda miti kwa lengo la kuboresha na kutunza mazingira nchini.
Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Meneja DAWASA Mabwepande, Ndugu HARUNA TARATIBU ameelezea umuhimu wa kupanda miti katika eneo hilo kama hatua mojawapo ya kutunza mazingira pamoja na vyanzo vya maji na pia kuzuia mmomonyoko wa udongo pamoja na kuboresha muonekano wa maeneo ya kutolea huduma za maji.
"Pamoja na agizo la Waziri Mkuu Mhe Kassim Majaliwa (Mb) kuzitaka Taasisi na Wananchi wote kwa ujumla tupande miti rafiki wa mazingira, sisi kama DAWASA Mkoa wa kihuduma Mabwepande tumeona tuje kupanda miti katika eneo hili la Tenki la Malolo ili kuboresha mazingira ya hapa pamoja na kutunza chanzo chetu cha maji" alisisitiza.
Zaidi ya miti 1000 imepandwa na watumishi wa Mamlaka ikiwemo miti ya matunda, Mti ya kivuli pamoja na Maua katika maeneo mbalimbali ya kihuduma ya Mamlaka.
Social Plugin