Mkuu wa wilaya ya KwimbaJijini Mwanza Ng'wilabuzu Ludigija amewataka wakazi wa wilaya hiyo kuhakikisha wanalala kwenye vyandarua viilivyoyolewa na serikali ili kujikinga na ugomjwa hatari wa Malaria kwasababu ni miongoni mwa Magonjwa yanyasababisha vifo vingi
Ludigija ametoa maelekezo hayo wakati wa uzinduzi wa zoezi la kugawa vyandarua vyenye viatilifu zaidi ya elf 12 katika mpango wa serikali wa kudhibiti Malaria Kwa watoto wadogo wenye umri chini ya mwaka mmoja na Kwa Makundi Maalumi kama vile Wajawazito wazee wenye umri miaka 60 na kuendelea, watoto wenye umri chini ya miaka 5 wanapoenda kutibiwa malaria, wanaoishi na Virusi vya Ukimw na wanaolazwa kutokana na malaria
Vyandarua hivi vitatolewa kwa mzunguko wa miaka miwili kwa makundi hayp na vina nembo ya MSD ikiwa ni mkakati wa Serikali ya awamu ya sita katika mpango wake wa kutokomeza malaria ifikapo mwaka 2030 na kuongeza umiliki wa vyandarua kwa jamii angalau 80%.
Aidha Amewasihi kuachana na Imani potofu juu ya vyandarua hivyo vinavyotolewa bure na serikali kwasababu Ina lengo la kuwalinda wananchi wake dhidi ya ugonjwa wa Malakeria hivyo amewataka wakazi hao kuwapuuza wanaojaribu kupotosha kuhusu vyandarua hivyo.