*************
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Maji safi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) Bw. Kiula Kingu ameendelea na ziara yake katika Mikoa ya Kihuduma ya DAWASA na Mitambo Kwa lengo la kuongea na Watumishi na kuhimiza uwajibikaji mahala pa kazi.
Katika ziara yake, Leo Aprili 14,2023 amekutana na Watumishi wa Mtambo wa kuzalisha maji Ruvu Juu, na mikoa ya kihuduma ya DAWASA Mlandizi na DAWASA Kibaha na kuendelea kusisitiza kufanya kazi kwa bidii na kutoa huduma bora kwa Wateja ambao ndio wanaowezesha Mamlaka kuwa mapato ya uhakika ya kuweza kujiendesha. Amesisitiza kuwa matokeo chanya ya uwajibikaji ndio yatakayoijenga kesho nzuri ya DAWASA .
'Hapa tulipo kumetokana na watu waliofanya kazi kwa bidii na ndio maana leo hii ni njema kwetu sote, nasi yatupasa kujituma na kuwa wabunifu ili kuifanya kesho yetu kuwa njema zidi kuliko leo'' alisisitiza Kiula
Licha ya kuzungumza na Wafanyakazi wa mikoa ya kihuduma, Kaimu Mtendaji Mkuu pia ametembelea miradi mbalimbali ya maji inayoendelea kutekelezwa katika mkoa wa Kibaha ukiwemo mradi wa Maji Boko mnemela na mradi wa Maji Pangani ambao upo katika hatua za utekelezaji.
Social Plugin