Mbunge wa Vitimaalum (Chadema), Esther Matiko ameomba serikali kuipa fedha za kutosha Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi.
Akichangia Aprili 6, 2023 bungeni mjadala wa makadirio ya mapato na matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2023/24, Mbunge huyo amesema Ofisi hiyo ina majukumu muhimu nchini ya kukuza staha kazini, Programu ya Taifa ya Kukuza Ujuzi na Mfuko wa Maendeleo ya Vijana.
Amesema ni muhimu bajeti inayopitishwa na bunge itolewe ipasavyo ili majukumu hayo yatekelezwe kwa ufanisi.
“Tafiti zinaonesha vijana 900,000 wanaingia kwenye soko la ajira lakini vijana kati ya 50,000 hadi 60,000 hivyo vijana zaidi ya 800,000 hawana ajira, hii ni Wizara muhimu sana ambayo serikali inapaswa kuwekeza fedha ili kusaidia vijana na watu wenye ulemavu,”amesema.
Social Plugin