SHEIKH WALID KAWAMBWA AIPONGEZA PUMA ENERGY TANZANIA KWA KUWAUNGANISHA WATANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania, Fatma Abdallah, akiwashukuru wageni waalikwa mbalimbali baada ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo, Dar es Salaam, Miongoni mwa wageni waaalikwa kwenye futari hiyo ni Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa.
*******************

Na Mwandishi Wetu

KAIMU Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa ameipongeza Kampuni ya Puma Energy Tanzania kwa kuwaunganisha Watanzania kupitia programu zake mbalimbali za kibiashara.

Amesema kampuni hiyo inajali kazi zake, kwa sababu ni chombo cha kibiashara na moja ya utaratibu wa biashara ni kuvuta soko ambalo halipatikani bila kutanguliza mapenzi ya dhati ya shughuli zake.

Sheikh Walid ametoa pongezi hizo, wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na kampuni hiyo, Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wageni wadau mbalimbali huku kwa upande wa Puma wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wake Fatma Abdallah na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma Energy Tanzania Dk. Suleiman Majige.

Amesema walichokifa Puma Energy Tanzania, kimeonesha wameelewa maagizo ya Mwenyezi Mungu ya kutaka watu kuishi pamoja, huku akisisitiza kampuni hiyo inajali kazi zake.

“Niwapongeze Puma Energy Tanzania, kwa wakati huu tuliokuwepo wa Mwezi wa Ramadhan, ambao Mwenyezi Mungu anatuagiza tufanye mengi ya kheri yanayomridhisha yeye,” amesema.

Amesisitiza kwamba kampuni hiyo inajali kazi zake kwa sababu ni chombo cha kibiashara na moja ya utaratibu wa kibiashara ni kuvuta soko ambalo halipatikani bila kutanguliza mapenzi ya dhati kwa shughuli zake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Puma Energy Tanzania, Dk. Suleiman Majige, alisema wanaendelea kuiombea kampuni hiyo kwani ni mali ya Watanzania, iendelee kufanya kaza vizuri.

Pia, Dk. Majige ameishukuru Menejimenti ya Puma Energy Tanzania kwa kazi walioifanya ya kuwaunganisha na kuwakaribisha katika hafla hiyo, pamoja na kuwatakia mfungo mwema wa Ramadhani inayoendelea.

Aidha amewataka kuwa karibu na Mungu katika kipindi cha mwezi mtukufu wa Ramadhani ambao ni muhimu kumuomba Mungu kila wakati aendelee kuleta neema na mapenzi mema.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah(wa kwanza kulia), Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma Energy Tanzania Dk . Suleiman Majige ( wa pili kulia) wakibadilishana mawazo na Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa( kushoto) wakati wa hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni hiyo jijini Dar es Salaam

Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa akitoa salamu kwa wageni waalikwa mbalimbali waliohudhuria hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni ya Puma Energy Tanzania .Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam wakiongozwa
Kaimu Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Kawambwa (katikati) waliokaa mbele akiwa katika picha ya pamoja na maofisa mbalimbali wa Kampuni ya Puma Energy Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji Fatma Abdallah ( wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Puma Energy Tanzania Dk Suleiman Majige ( wa pili kulia)


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post