Naibu Katibu Mkuu wa Wazara ya Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Dkt.Ally Possi akizungumza wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Utafutaji na Uokoaji yaliyoratibiwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO) na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
**************
-Dkt.Possi abainisha uwekezaji wa Sekta ya Usafirishaji wa Majini na Anga
Na Chalila Kibuda,
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi -Uchukuzi Dk.Ally Possi amesema kuwa serikali imewekeza kwa kiwango kikubwa katika sekta ya usafirishaji wa Majini na Anga ambapo uwekezaji huo unatakiwa kuwa na wataalam wa utafutaji na Uokoaji wa ajali za katika sekta hiyo.
Dk.Possi ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku Tano yaliyoratibiwa na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) na Shirika la Bahari Duniani(IMO) yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Amesema mafunzo hayo ni muhimu kwa wataalam kuwa na ujuzi wa kukabiliana na majanga na ajali za vyombo vya majini na anga ambapo hilo ndilo linatambulisha usalama wa nchi kwenye sekta ya usafirishaji na kuendelea kupata meli na ndege za kuleta watalii wengi.
Dk.Possi amesema mafunzo katika utafutaji na Uokoji wa ajali na majanga mengine katika usafirishaji wa majini utaaksi dhamira ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
Possi amesema mafunzo kwa wataalamu hao pamoja na mambo mengine watakayoyapata yataendelea kuwaimarisha na kuwajengea uwezo katika vituo vyao vya kazi.
Amesema mafunzo hayo ni muhimu hususani kwa watalamu wote ambao wanafanya kazi na TASAC kwa kutambua uwepo wa majanga na ajali ambazo zinajitokeza hususani kwenye usafirishaji wa majini.
"Mafunzo haya ni muhimu kwa kutambua kwamba maeneo yetu ya sekta ya Anga na Majini yanakuwa salama .hivyo mafunzo hayo haya ni muhimu kwani watalaamu wetu watapata ujuzi wa kisasa na lazima tutambue kuwa Nchi na Bara letu linakabiliwa na changamoto gani na katika mada zitakazotolewa katika mafunzo wahakikishe wanakuja na suluhisho ,"amesema Dkt Possi
Ameongeza kwamba anafahamu nchi zetu zinakosa vifaa vya kisasa lakini pia mambo ya kibajeti, hivyo watalamu wakae wafundishane na waje na mapendekezo ambayo Serikali wataendelea kuyachukua na kimsingi Serikali wana mikataba ya kimashirikiano ya Kimataifa ambayo pia kuna masuala ya utafutaji na Uokoaji kupitia sekta za Anga na Majini.
Amesema lazima wataalamu wapate ujuzi wa kutosha kwani hata zinapojitokeza changamoto wawezcj kukabiliana nazo
Dkt.Possi ameongeza kuwa nchi isipokuwa na vyombo au utaratibu wa Utafutaji na Uokoaji katika sekta ya Anga na Majini basi itakuwa na changamoto na kuhatarisha sekta nyingine.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa TASAC Kaimu Abdi Mkeyenge amesema kuwa lengo kubwa la mafunzo hayo yatakayotolewa na wakufunzi wa Kimataifa kutoka Shirika la Bahari Duniani (IMO) yatawaimarisha wataalam wetu kwenye shughuli za Utafutaji na Uokoaji wakati wa majanga au ajali zinapotokea nchini.
Amesema kuna vigezo mbalimbali vilivyowekwa vya kimkataba vya Shirika la Bahari Duniani (IMO) ulioingiwa mwaka 1979 ambao moja ya vigezo hivyo ni masuala ya Utafutaji na Uokoaji kwa ajali zinazotokea majini, hivyo basi Tanzania kama nchi wanachama hawanabudi kutekeleza kwani walishauridhia na ulianza kufanya kazi tangu mwaka 1985.
Mkeyenge amesema wao wamekuwa ni wanachama kwa muda mrefu lakini pia kuna vitu ambavyo vilikuwa bado vinakwenda kwa kasi ambayo haikuwa inaridhisha, hivyo wameona huu ni wakati mahususi kuimarisha katika maeneo yote ikiwemo kuwajengea uwezo wa watalaam kwendana na viwango vilivyowekwa na shirika hilo kwani wasipotekeleza matakwa ya mkataba huo wanaweza wakawa wanapata changamoto panapojitokeza majanga kama hayo .
Pamoja na mambo mengine amesema cha kwanza wanachoweza kukifanya ni kuwawezesha wadau wote ambao wanahusika na masuala ya utafuataji na uokoaji maeneo ya bahari na ndio maana kuna vyombo vya ulinzi vinavyohusika na usalama vipo."Kwa hiyo mafunzo hayo yatakwenda kuwawezesha watu hao kuwa wazuri katika maeneo yao.
Ameongeza mafunzo mbalimbali huwa yanafanyikia japo kutoka katika Shirika la bahari Duniani ni kwa ufinyu sana kwasababu ni tabu pia kuwapata lakini inategemea na nguvu ya uhamasishaji kama nchi, hivyo sasa wameamua kutoka na kwenda kuomba fursa ili zije nchini hata kama mafunzo hayo yakiwa yanafanyikia kama ya kikanda.
"Lakini tunahitaji yafanyike hapa nchini ili uelewa uwepo kwa umma wote au wadau katika maeneo hayo, pia mafunzo kama hayo wanategemea yatafanyika tena Juni mwaka huu."
Nahodha wa Usimamizi wa Majini wa Kituo cha Utafutaji na Uokoaji wa TASAC Alex Katama akizungumza kuhusiana na mafunzo hayo katika kuongeza uwezo wa kukabiliana wakati majanga ya ajali kwenye Utafutaji na Uokoaji , jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wazara ya Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Dkt.Ally Possi akiwa katika picha ya pamoja Vyombo vya Ulinzi vya Uokoji mara baada kufunguliwa kwa Mafunzo ya Utafutaji na Uokoaji yaliyoratibiwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO) na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Naibu Katibu Mkuu wa Wazara ya Ujenzi na Uchukuzi-Uchukuzi Dkt.Ally Possi akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa mafunzo ya Utafutaji na Uokoaji mara baada kufunguliwa yaliyoratibiwa na Shirika la Bahari Duniani (IMO) na Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) yaliyofanyika Katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.
Social Plugin