Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye akiwa pamoja na Meneja Mkaazi wa CAMARA Education Tanzania Bw. Dayani Mbowe wakisaini mkataba wa makubaliano katika kutekeleza kwa pamoja miradi ya kuwezesha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye mashule kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye akiwa pamoja na Meneja Mkaazi wa CAMARA Education Tanzania Bw. Dayani Mbowe wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano katika kutekeleza kwa pamoja miradi ya kuwezesha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye mashule kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye akiwa pamoja na Meneja Mkaazi wa CAMARA Education Tanzania Bw. Dayani Mbowe wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kusaini mkataba wa makubaliano katika kutekeleza kwa pamoja miradi ya kuwezesha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye mashule kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye akizungumza mara baada ya TEA kuingia Makubaliano na Kampuni ya CAMARA Education Tanzania katika kutekeleza kwa pamoja miradi ya kuwezesha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye mashule kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye akizungumza mara baada ya TEA kuingia Makubaliano na Kampuni ya CAMARA Education Tanzania katika kutekeleza kwa pamoja miradi ya kuwezesha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye mashule kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.
Meneja Mkaazi wa CAMARA Education Tanzania Bw. Dayani Mbowe
akizungumza mara baada ya TEA kuingia Makubaliano na Kampuni ya CAMARA Education Tanzania katika kutekeleza kwa pamoja miradi ya kuwezesha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye mashule kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Hafla hiyo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
MAMLAKA ya Elimu Tanzania TEA na Kampuni ya Camara Education Tanzania wameingia makubalino maalumu ya kushirikiana katika kutekeleza kwa pamoja miradi ya kuwezesha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) kwenye shule za msingi na sekondari kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.
Katika makubaliano hayo, awamu ya kwanza Kampuni ya Camara Education Tanzania imetenga kiasi cha shilingi Milioni 50 ambayo imelenga kutekeleza kwa pamoja miradi ya kusimika na kusambaza vifaa vya TEHAMA mashuleni.
Akizungumza katika hafla hiyo ambayo imefanyika leo Aprili 12,2023 kwenye Ofisi za TEA Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mkuu wa TEA Bi. Bahati Geuzye amesema,TEA inaungana na CAMARA Education Tanzania kuweka na kuunganisha miundombinu ya TEHAMA mashuleni ili kuwaandaa wanafunzi katika ngazi zote kuendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa miaka mitano 2021/22 - 2025/26 ambao umejikita katika kukuza ujuzi kupitia hatua za kutatua changamoto ya upungufu wa ujuzi tepe (soft skills) (hususan maarifa, ubunifu, uhimilivu, kujituma na mtazamo chanya) na kutowiana kwa ujuzi unaohitajika katika soko la ajira na ule unaotolewa katika taasisi za elimu na mafunzo kwa wanaotafuta kazi.
Amesema kuwa, Taasisi au watu wanaochangia kupitia TEA wanatambuliwa rasmi kwa kupewa cheti maalum cha utambuzi ambacho wanaweza kutumia kuomba nafuu ya kodi kwa Kamishna wa Kodi ya Mapato Nchini (TRA) kama ilivyoanishwa katika kifungu cha 12 cha Sheria ya Mfuko wa Elimu ya mwaka 2001 pamoja na Kifungu cha 16 cha Sheria ya Mapato ya mwaka 2004.
Aidha ameipongeza CAMARA Education Tanzania na wadau wote ambao wamekuwa wakitoa michango katika sekta ya elimu kupitia TEA, na wadau wengine wote kwa kushirikiana nao katika kusukuma mbele jitihada za Serikali za kuboresha miundombinu ya elimu nchini.
"Tunawahakikishia wadau wote wa sekta ya elimu kuwa TEA iko tayari kushirikiana nao katika kuboresha miundombinu ya Elimu, hivyo tunawakaribisha sana kutoa michango kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa. TEA tutaendelea kusimamia kikamilifu fedha zinazowekezwa katika Mfuko wa Elimu na kuhakikisha kuwa miradi inatekelezwa kwa ufanisi na thamani ya fedha inakuwepo". Amesema Bi.Geuzye.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa CAMARA Education Tanzania Bw. Dayani Mbowe amesema wamekuwa wakishirikiana na TEA kwa muda mrefu kwa kufanya miradi ya TEHAMA ambapo hadi sasa washatekeleza katika shule 300 nchini.
Amesema katika miradi hiyo ilihusisha kusambaza vifaa vya TEHAMA, kufunga miundombinu ya TEHAMA kwenye shule pamoja na kuwajengea walimu uwezo wa kutumia vifaa hivyo .
Pamoja na hayo amewahimiza wadau wengine kushirikiana na TEA wachangie katika mfuko wa elimu ili kufanikisha miradi ambayo imekuwa ikiendelezwa na Mamlaka hiyo katika uboreshaji wa elimu bora nchini.
Social Plugin