Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TMDA YAENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI SAHIHI YA DAWA NA VIFAA TIBA KWA WANAFUNZI WA SHULE ZA SEKONDARI DAR ES SALAAM


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MAMLAKA ya Dawa na Vifaa Tiba TMDA imeendelea kutembelea katika shule za Sekondari kwaajili ya kutoa elimu kuhusu majukumu yanayofanywa na Mamlaka hiyo katika kuhakikisha jamii inaelewa matumizi sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba pamoja na kupunguza madhara yanayojitokeza kwa watumiaji wa Dawa na Vifaa Tiba.

Akizungumza katika zoezi hilo jana  Aprili 14,2023 Afisa wa TMDA, Bw.Boniface Likati amesema wameamua kupita katika mashule kwaajili ya kuitambulisha TMDA kuelezea majukumu ambayo yanafanywa na TMDA ambayo ni kulinda afya ya jamii kwa kuangalia ubora, usalama na ufanisi wa Dawa, Vifaa Tiba na vitendanishi.

Kumekuwa na matumizi yasiyo sahihi ya Dawa na Vifaa Tiba hivyo kupelekea madhara katika jamii na taifa kwa ujumla, kwahiyo tukaona ni vizuri kupita katikashule za Sekondari tukiamini hawa watakuwa mabalozi wazuri kuhamasisha matumizi sahihi ya dawa

Kwa sasa kumekuwa na changamoto kubwa ya watu kutokuzingatia matumizi sahihi ya Dawa ambapo inapeleka kuwa na changamoto hasa katika afya zetu hata katika suala zima la Serikali ambapo inajikuta inaingia gharama kubwa kwaajili ya kuagiza Dawa na Vifaa Tiba.

Matumizi yasiyo sahihi ya Dawa yanaweza kupelekea usugu wa dawa na kushiindwa kutibu tatizo ambalo awali lilikuwa linatibiwa na dawa hizo na hii inachangia na watu kutokuzingatia kile ambacho wanaambiwa na wataalamu.

Pamoja na hayo amewataka wananchi kuhakikisha wanapoenda kununua dawa wanaangalia muda wa matumizi unaisha lini ili kuweza kuepuka madhara ya kiafya yatakayojitokeza kwa mtumiaji wa dawa hizo.

Kwa upande wake Afisa Elimu ,Vifaa na Takwimu kutoka Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam Mwl. Mohammed Katundu amesema Halmashauri ya jijini Dar es Salaam linajumla ya shule 114 ambapo mpaka sasa wameweza kutembelea 23 sawa na wanafunzi elfu 20,231 na walimu 766 ambao wote wamepata elimu sahihi ya matumizi sahihi ya dawa.

Aidha ameipongeza TMDA kwa kufanya elimu hiyo kwani inawasaidia kundi la wanafunzi ambalo limekuwa likinunua dawa bila maelekezo ya daktari, na kupitia elimu hiyo watapata ushauri wa daktari kabla ya matumizi ya dawa na hatimae kuepuka na matumizi ya dawa bila kuonana na daktari.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Minazi Mirefu Averine Chugulu amewapongeza viongozi husika kuruhusu TMDA kuwafikia walimu na wanafunzi katika kutoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya dawa na kuzingatia muda wa matumizi ya dawa kwa kuzingatia maelekezo ya daktari.

Na Mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Minazi Mirefu, Hossiana Mshanga Amesema wamepata fursa ya kupata elimu ya matumizi sahihi ya dawa ili kuleta afya bora kwa watumiaji, pia amepata uelewa kuhusu majukumu mengine ya TMDA hasa kusajili na kutoa Vibali kwa majengo ambayo yanatengeneza na kuuza Dawa, Vifaa Tiba na Vitenganishi

“Nimepata fursa kujua majukumu mengi ya TMDA yakiwemo kukagua shehena mbalimbali ambazo zinahifadhi Dawa katika maeneo ya forodha na kwenye maghara mbalimbali pia wanatumika kudhibiti au kuratibu matangazo mbalimbali yanayohusu bidhaa za Dawa”. Amesema

Amejifunza kuhusu umuhimu wa kupima pindi unapojisikkia unaumwa ili kuweza kupata ushauri wa daktari na kupatiwa dawa na matumzii sahihi ya dawa ambazo wamepatiwa na kuepuka matatizo yatokanayo na matumzi yasiyosahihi ya dawa.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com