Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAUGUZI HOSPITALI YA RUFAA YA BOMBO WAFUNDISHWA NAMNA YA KUPIMA USIKIVU WA WATOTO WANAPOZALIWA

 Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt Edwin Liyombo akizungumza na waandishi wa habari ambao hawapo pichani kuhusu mafunzo walioyatoa kwa wauguzi waliopo katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo namna ya kupima usikivu wa watoto wadogo wanapozaliwa ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi na tija kubwa kwa wananchi wanaowahudumia

Muuguzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Prisca Massawe kushoto akimpima usikivu mtoto aliyezaliwa katika hospital hiyo wakati wa mafunzo ya kuwafundisha namna ya kupima usikivu kwa watoto wachanga wanapozaliwa kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Hamisi Shaban Mtitho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili

Muuguzi wa Hospital ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga Bombo Prisca Massawe kushoto akimpima usikivu mtoto aliyezaliwa katika hospital hiyo wakati wa mafunzo ya kuwafundisha namna ya kupima usikivu kwa watoto wachanga wanapozaliwa kulia ni mkufunzi wa mafunzo hayo Hamisi Shaban Mtitho kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili



WAUGUZI katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga-Bombo wamefundishwa namna ya kupima usikivu wa watoto wadogo wanapozaliwa ili kuweza kutoa huduma hiyo kwa ufanisi na tija kubwa kwa wananchi wanaowahudumia

Akizungumza wakati wa mafunzo hayo mwishoni mwa wiki ,Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Masikio, Pua na Koo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt Edwin Liyombo alisema kwamba wameamua kuwafundisha wauguzi program ya kupima usikivu kwa watoto wanaozaliwa ili kuweza kuwasaidia watoto wanaokuwa na shida hiyo pindi wanapozaliwa.

Alisema kwa sababu imeonekana kuna watoto wengi wanajulikana wana matatizo ya usikivu na wanashindwa kuongeza pindi wanapokuwa na umri wa kuanza kwenda shule ikiwemo wanaozaliwa hawawezi kuongea hivyo mpango huo unasaidia kugundua mtoto pale anazaliwa mpaka mwezi mmoja.

Aidha alisema kwa sababu kuna mashine maalumu ya kuwapima kama wana matatizo na wakibainika mapema inawasaidia kuweza kuona namna ya kulipatia ufumbuzi.

“Tunawafundisha wauguzi jinsi ya kufanya uchunguzi na baadae itakwenda nchi nzima kwani hawa wanaowafundisha baadae watakuwa walimu na kufundisha wengine lakini tutawaleta mashine ndogo itakayotumika kupima watoto wanapozaliwa”Alisema

Hata hivyo alisema kwamba wanaomba watu wajitokeze wakati wa mpango huo wa kupima usikivu huku akieleza kwamba katika zoezi lao wamepima watoto 20 wengi hawana matatizo kadri watakavyopima wengi watajua hali ipo vuzri na hivyo kuisaidia wizara kupanga bajeti ili kuona namna ya kuwasaidia.

Katika hatua nyengine Dkt Edwin alisema kwamba takwimu zinaonyesha kwamba kati wa watu 100 watu 7 wana tatizo la usikivu na watoto wadogo na ndio sababu Hospitali ya Taifa ya Muhimimbiili walianzisha program ya kuweka kipandikizi kwa ajili ya kusikia ambayo tokea mwaka 2017 mpaka sasa watoto 57 wamekwisha kufanyiwa.

Alieleza kwamba watoto wengi wanakuwa na matatizo wakati wanazaliwa au wakiwa na umri mdogo wameona wakiwagundua mapema inasaidia kufuatilia kuona ni sababu zipi zinapelekea kuwepo kwa hali hiyo kwa watoto ili kuweza kuzuia lisiweze kujitokeza.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com