Waziri wa Utalii Mhe. Mohamed Mchengerwa leo Jumapili April 16, 2023, Ametua Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa) na kuwataka watumishi wa Mamlaka kuchapa kazi kwa weledi na nidhamu na zaidi kuvitangaza vivutio vya utalii vilivyoko katika eneo hilo kwa kasi na ubunifu. Tanapa inasimamia Hifadhi za Taifa 22 ambazo ni sawa na asilimia 11 ya eneo lote la Tanzania.
Katika ziara hiyo ameongozana na watendaji wakiongozwa na Katibu Mkuu, Dkt. Hassan Abbasi na Naibu Katibu Mkuu, Bw. Anderson Mutatembwa.
Viongozi wa Tanapa wameeleza kuwa kutokana na filamu ya Royal Tour mapato na idadi ya watalii vimeongezeka kuliko wakati wowote katika historia ya hifadhi hizo.
Social Plugin