Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

WAZIRI MKUU KUONGOZA WABUNGE SEMINA YA WADAU SEKTA YA MAJI

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa anatarajia kuwa mgeni rasmi katika semina ya siku moja ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wizara ya Maji kitakachofanyika siku ya Ijumaa, Aprili 28., 2023.

Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amefika mapema ofisi ya Waziri Mkuu Bungeni Dodoma kwa mazungumzo na kutumia nafasi hiyo kumualika rasmi na kumpa muhtasari na muelekeo wa kikao kazi hicho muhimu kwa Sekta ya Maji Nchini.

Semina hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Bunge wa Pius Msekwa kuanzia saa 7 Mchana na litarushwa mubashara kupitia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Kituo cha Habari cha Taifa TBC1.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com