Na Munir Shemweta, WANMM
Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi imewafuturisha watumishi wake waliopo Wizarani na ofisi ya Kmishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula na Naibu wake Geofrey Pinda waliwaongoza viongozi wa wizara hiyo kujumuika na watumishi katika futari iliyofanyika tarehe 3 April 2023 jijini Dodoma.
Akizungumza wakati wa futari hiyo, Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula aliwaeleza watumishi kuwa, uamuzi wa kuandaliwa futari ya pamoja unalenga kuwaweka pamoja watumishi wa wizara hususan kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na kwa rezma.
‘’Uamuzi wa kuandaa futari ya pamoja unalenga kuwaweka pamoja watumishi wa wizara yetu na ninaomba tuwe na umoja na kushirikiana katika kazi zetu’’ alisema Dkt Mabula.
Naibu Waziri wa Ardhi Geofrey Pinda alishukuru uamuzi wa Wizara kukutanisha pamoja watumishi kuanzia ngazi ya chini hadi juu jambo alilolieleza kuwa ni nadra sana kutokea watumishi kukutana kwa wakati mmoja kuanzia kada ya chini hadi juu.
‘’Nishukuru uamuzi wa kuwakutanisha watumishi wa sekta ya ardhi pamoja maana ni nadra sana watumishi wa wizara kuanzia kada za chini hadi juu kukutana kwa mara moja’’ alisema Pinda
Kwa upande wake, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anthony Sanga alihimiza watumishi wa sekta ya ardhi kuwa na umoja wakati wote wa utendaji kazi.
Aidha, aliwaeleza watumishi wa wizara ya ardhi kuwa, wizara hiyo kwa sasa iko kwenye juhudi za kuboresha mifumo yake ya ulipaji kodi ya pango la ardhi ambapo alieleza kuwa mfumo huo utakapokamilika wamiliki wa ardhi nchini watakuwa wakipata ujumbe utakaowawezesha kulipa kodi bila kufika ofisi za ardhi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuandaa futari ya pamoja ya watumishi wake tangu serikali ilipohamia rasmi mkoani Dodoma.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula akizungumza wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi iliyofanyika jijini Dodoma tarehe 3 April 2023. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Lucy Kabyemera na katikati ni Kaimu Mkuu wa Utawala na Rasilimali Watu Wizara ya Ardhi Isabela Chilumba.
Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anthony Sanga akiwaongoza watumishi wa wizara ya ardhi kupata futari ya pamoja jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Watumishi wa Wizara ya Ardhi wakifuatilia hotuba ya Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt Angeline Mabula wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara hiyo jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Geofrey Pinda akizungumza wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Kamishna wa Ardhi nchini Nathaniel Methew Nhonge akitoa neon la shukran wakati wa futari ya pamoja ya watumishi wa wizara ya ardhi jijini Dodoma tarehe 3 April 2023.
Social Plugin