Polisi mkoani Songwe limemkamata Aloyce Nyabwanzo (53), Mkazi wa Kitongoji cha Kikamba, Kijiji cha Kapalala wilayani Songwe kwa tuhuma za kuwaua wajukuu zake wawili kwa kuwapasua mafuvu ya kichwa na mchi wa kutwangia hadi ubongo kumwagika.
Watoto waliouawa ni Jackson Chacha (2) na George Chacha (5) wote wakazi wa kitongoji cha Iwindu- Kikamba katika Kijiji cha Kapalala na walikuwa wakilelewa na mtuhumiwa.
Inaelezwa kuwa mtuhumiwa alitumia mbinu ya kuwavizia wajukuu zake hao wakati wanatoka chumbani kwao kumfuata bibi yao sebuleni aliyekuwa anajaribu kuzuia mlango usivunjwe na mtuhumiwa huyo baada ya kuanzisha vurugu nyakati hizo za usiku.
Social Plugin