Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

MRINDOKO : HATUTAKUBALI KUONA MTU ANALETA MGOGORO CCM....TUKEMEE USHOGA, USAGAJI

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Kamati ya Utekelezaji ya Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini imekemea makundi ndani ya chama na migogoro ikisisitiza kuwa kamwe haitakubali kuona mtu yeyote analeta mgogoro katika chama hicho.

Akizungumza leo Jumamosi Mei 20,2023 wakati wa ziara ya kamati hiyo katika kata ya Chamaguha, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko amewataka wanaCCM kupendana na kushikamana na kuwa na umoja ili kujenga chama.

“Naomba wanaCCM tupendane na kama hatutaelewana tutapoteza dola. Mkiona mtu analeta mgogoro, heri aondoke kuliko kupoteza dola, sisi tumezoea kuwa na dola hatuwezi kukubali dola ipotee. Mtu yeyote unayeona analeta longolongo ya kutaka tupoteze dola aondoke CCM”,amesema Mrindoko.

Mwenyekiti huyo wa Jumuiya ya Wazazi pia amekemea vitendo vya ushoga na usagaji katika jamii akisema hayo ni mambo ya aibu na ya ajabu hivyo kuwataka wazazi kusimama imara katika malezi ya watoto ili kukabiliana na mmonyoko wa maadili.

“Tuwalindeni watoto, tuwalindeni wajukuu zetu tuepuke tabia mbovu zinazoletwa na mataifa ya nje. Mtoto akirudi kutoka shule mkague maana dunia imeharibika. Tuwe makini kwa watoto wetu, tuwe makini kwa mabinti zenu mambo yameharibika. Huu mchezo ukiendelea tutakuwa na viongozi kweli?.

“Hawa wamama wanaosagana wametukosa sisi wanaume?? Mababa tupo akina mama msihangaike kusagana.  Eti wanaume wanalawitiana mna akili kweli”,amesema Mrindoko.

Naye Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi amewataka wanandoa kupendana na kushirikiana katika malezi ya familia.

“Kupigana siyo dili wanandoa pendaneni, furaha ya ndoa inatakiwa iwepo kila siku na tuachane na vitendo vya ubakaji na ulawiti ndani ya famila zetu.Ukiona babu anamuita mjukuu wake mke, shtuka , kwani wapo wababu wanawafanyia ukatili watoto”,amesema Kibabi.

“Tukemee ushoga , siku hizi unakuta mme wako kumbe naye ni mke wa mwanaume mwenzake, mambo ya ajabu sana haya, lazima tuyakemee”,ameongeza Kibabi.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Fue Mrindoko akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023

Katibu wa Jumuiya ya Wazazi CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini, Doris Yotham Kibabi akizungumza na wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha Manispaa ya Shinyanga leo Jumamosi Mei 20,2023

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko ambaye ni diwani wa kata ya Chamaguha akizungumza kwenye kikao cha wanachama na viongozi wa CCM Kata ya Chamaguha

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com