Hakimu mkazi Mahakama ya wilaya ya Tarime Vincencia Balyaruha
Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntenjele
Mkurugenzi wa Asasi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Koshuma Mtengeti
Na Frankius Cleophace Mara
Mahakama ya wilaya ya Tarime Mkoani Mara imesema kuwa itaendelea kutoa kupaumbele kesi zinazohusu masuala la Ukatili pamoja na kesi za watoto ili zisichukue muda mrefu katika utoaji maamuzi yake.
Hayo yamebainishwa na Hakimu mkazi Mahakama ya wilaya ya Tarime Vincencia Balyaruha kwenye mkutano wa mwaka wa wadau wa haki za ulinzi wa mtoto wilaya ya Tarime kilichoandaliwa na Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF Tarime.
Hakimu alisema kuwa kwa sasa mahakama ya watoto inakaa kila Alhamisi pia mara nyingi kesi zinazohusu watoto zikiwemo za ukatili zinapewa kipaumbele ili ziweze kusikilizwa na kumalizika mapema.
“Tumekuwa tukikutana mara kwa mara ili kuweza kuweka mikakati ya kumalizakesi hizi mapema licha ya changamoto ya ushahidi lakini bado hatujakata tamaa”, alisema Hakimu.
Pia Hakimu aliongeza kuwa suala la kumaliza kesi kiundugu bado linawapa changamoto kwani wahanga wa ukatili wamekuwa wakikwepa kutoa ushahidi nawakati mwingine kuacha kuudhuria mahakama sisi kwetu ni changamoto kubwa.
"Pia nasisitiza sana jamii kuendelea kuhimalisha ulinzi kwa watoto ili kupunguza vitendo vya ukatili kwenye jamii mfano watoto wadogo chini ya miaka 08 pia na watoto wengine lazima walindwe",alisema.
Koshuma Mtengeti ambaye ni mkurugenzi wa Asasi ya Jukwaa la Utu wa Mtoto CDF alisisitiza jamii kuendelea kulinda watoto juu ya ukatili nakuwapa haki zao za msingi mfano kupatiwa elimu, mavazi pamoja na muda wa kuchezo jambo hilo litazidi kuwajengea uwezo mkubwa.
“Vyombo vya Habari mnanafasi kubwa kwenye jamii hebu endelea kutoa elimu ikiwemo elimu ya ulinzi na usalama kwa watoto ili kupunguza ukatili ambao umekuwa ukitokea kwenye jamii zetu.” alisema Koshuma.
Naye Kaimu Afisa mkurugenzi Halmashauri ya wilaya ya Tarime Sylivanus Gwiboha alisema kuwa serikali inaendelea kujipanga na kuweka mazingira rafiki kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia ili waendelee kupata msaada kwa wakati.
Aidha Mkuu wa wilaya ya Tarime Kanali Michael Mntenjele wakati akifunga kiako hicho cha mwaka alisema kuwa sasa mashirika yote wilayani Tarime yashirikiane kwa pamoja ili kutoa elimu juu ya madhara ya ukatili wa kijinsia.