Nusura Hassan Abdallah enzi za uhai wake
Na Abel Paul wa Jeshi la Polisi
Jeshi la Polisi Nchini Tanzania limesema kuwa limeona mjadala katika mitandao ya kijamii ikuhusiana na kifo cha Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma Bi. Nusura Hassan Abdallah kilichotokea huko Mkoani Kilimanjaro.
Akitoa taarifa hiyo leo mei 06,20223 msemaji wa Jeshi la Polisi Nchini kamishina msaidizi mwandamizi wa Polisi David Misime amesema kuwa taarifa hizo zimekuwa zikihusisha kifo hicho na ajali iliyotokea Jijini Dodoma Aprili 26,2023 ikimhusisha Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tamisemi (Afya) Mhe.Dkt. Festo Dugange ambapo zinadaiwa zimetokana na kipigo kutoka kwa mpenzi wake.
Msemaji wa Jeshi hilo amebainisha kuwa Jeshi la Polisi Tanzania lingependa kutoa ufafanuzi kuwa, Polisi Mkoa wa Kilimanjaro baada ya kuona taarifa hizo kupitia mitandao ya kijamii na sababu zinazotolewa,wameshaanza uchunguzi kwa watu mbalimbali,hospitalini alikotibiwa binti huyo ambapo amesema wanashirikisha Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali,Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) na wadau wengine wa haki jinai.
Aidha Jeshi hilo limetoa wito kwa mtu yeyote mwenye taarifa zilizosahihi na zenye ukweli asisite kutoa taarifa hizo ili kuharakisha uchunguzi wa tukio hilo.
Pia SACP Misime amesema kuwa Jeshi la Polisi Nchini linasisitiza kuwa Uchunguzi wa tukio hilo ukikamilika taarifa kamili ya kilichobainika kitatolewa kwa umma na kwa mujibu wa sheria,kanuni na taratibu za Nchi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Philip I. Mpango akizungumza na Naibu Waziri Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dkt. Festo Dugange tarehe 29 Aprili 2023 wakati alipofika hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Benjamin Mkapa kumjulia hali baada ya kupata ajali ya gari.
Dkt. Dugange alipata ajali usiku wa tarehe 26 Aprili 2023 wakati akiendesha gari yake binafsi Jijini Dodoma ambapo kwa sasa anaendelea kupatiwa matibabu katika Hospitali ya Rufaa ya Benjamini Mkapa.
Gari ya Serikali Vs Gari binafsi ya Mhe Dugange iliyopata Ajali