Afisa mtendaji mkuu wa benki ya CRDB Boma Rabilla akikabidhi hundi ya milioni 50 waandaaji wa maonyesho ya KARIBU KILL FAIR, Dominic Shoo wakwanza kulia na Tom Kunkler wapili kutoka kulia
Na Woinde Shizza, ARUSHA
Zaidi ya nchi 30 kutoka Duniani na makampuni zaidi ya 300 zinatarajia kushiriki maonyesho ya Karibu Kill Fair viwanja vya Magereza Kisongo jijini Arusha yanayotarajiwa kufanyika June 2 hadi 4, 2023
Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi mtendaji wa Kill Fair Promotion Limited Dominic Shoo amesema kuwa maonyesho hayo yanatumika pia kutangaza nchi ya Tanzania kwa sababu wanapotembea kutafuta masoko nchi zingine duniani wanatumia pia kuitangaza na kuwasihi watu waje katika maonyesho haya ili waweze kuona vivutio vilivyopo pamoja na kuonana na watanzania.
Shoo amesema kuwa ongezeko la watalii nchini Tanzania limechangiwa zaidi na kampuni ya Karibu Kill Fair ambapo amesema maonyesho hayo ni ya kimataifa hivyo yatashirikisha watu mbalimbali kutoka nchi 30 na wanatarajia kuona Tanzania ina nini ili waweze kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana hapa nchini .
Makamu mwenyekiti wa Tato Henry Kimambo amesema kuwa kuwa lengo kubwa la tukio hilo la maonyesho ni kuwezesha kuunganisha wadau wa sekta ya utalii kutoka nchini na nje ya nchi ya Tanzania kupelekea kuungana na mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan Kwa kuweza kufikisha watalii 500 mpaka kufikia mwaka 2025.
"Na ijulikane kuwa katika nchi ya Tanzania benki ya serikali ya crdb siyo mara ya kwanza kudhamini maonesho hayo na kulingana na takwimu kutoka benki kuu nchini mwaka 2022 baada ya ya biashara ya dhahabu kuingiza pesa nyingi Tanzania biashara inayofuatia ni hii ya utalii ambapo serikali imeweza kuingiza kiasi cha bilion 2.4 za kimarekani hii inaonesha namna ambavyo serikali inapata mapato"alisema
Afisa mtendaji mkuu wa benki ya CRDB Boma Rabilla ambao ni miongoni mwa wadhamini katika maonyesho hayo alisema kuwa wanajivunia kushiriki katika maonesho hayo kwani lengo la kushiriki ni kulenga kuinua sekta ya utalii,ukizingatia benki ya CRDB kuwa benki ya kwanza nchini kwa kuanzisha kadi maalum ya kuwezesha watalii kufanya malipo wakiwamo wafanyabiashara kunufaika na mikopo mbalimbali ya biashara.
Social Plugin