Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

DED KISHAPU APONGEZWA KWA USIMAMIZI MZURI UKUSANYAJI KODI


Viongozi wakiwa kwenye Baraza la madiwani halmashauri ya Kishapu
Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga Emmanuel Johnson Matinyi
Mkuu wa wilaya ya Kishapu, Modest Mkude

Na Sumai Salum - Kishapu
Baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Kishapu Mkoani Shinyanga kupitia kikao chake cha tatu cha mwaka wa fedha 2022/2023 limempongeza mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo Emmanuel Johnson Matinyi kwa ukusanyaji kodi mzuri na kufikia 92.2%.


Pongezi hizo zimetolewa leo Mei 10,2023 akisoma taarifa ya kwa niaba ya Mwenyekiti wa halmashauri ya Kishapu, diwani wa kata ya Selebugoro mhe. Ferdnand Mpogomi amesema halmashauri kupitia mapato ya ndani mwaka wa fedha 22/23 walikusudia kukusanya kiasi cha Tsh. Bill.3. 2 ambapo mpaka leo Mei 10 amekusanya Tsh Bilioni 2. 3


Mpogomi amesema, makusanyo hayo yameiwezesha halmashauri kutekeleza miradi yake ya maendeleo pamoja na ujenzi wa kituo cha afya kwa gharama ya Tsh. milioni 500 Huku ujenzi huo ukiwa kwenye hatua nzuri za ukamilishwaji.


"Matinyi anastahili pongezi kwani bado ni msimamizi bora wa mapato ya fedha za serikali iliyopelekea Kishapu tukapata hati Safi kwa mwaka wa fedha 2021/2022,lakini bado amesimamia ukamilishaji wa miradi ya maendeleo kwa wakati na kwa ubora unaostahili", ameongeza Mpogomi.


Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Kishapu Joseph Mkude amewataka madiwani kuendelea kushirikiana na watumishi kwa kila mtu asimamie mipaka yake kwa lengo la kuzia migogoro sehemu za kazi kwani itasaidia kuleta majibu na matokeo mazuri ya fedha zinazopatikana kwa mapato ya ndani na zinazoletwa kutoka serikali kuu.


Katika hatua nyingine Mkude amesema, madiwani wote wahakikishe wanahamasisha jamii kutunza mazingira,matumizi Bora ya ardhi,kuhifadhi taka mahali pale pamoja na ujenzi wa vyoo bora.


Hata hivyo kutokana na kuripotiwa kwa matukio mengi ya ukatili kwa watoto na wanawake sehemu mbalimbali nchini ikiwemo Kishapu ameitaka jamii na wazazi kuhakikisha wanalinda usalama wa watoto wao hata wakati mwenge wa uhuru unaotarajiwa kupokelewa kiwilaya Julai 27 mwaka huu.




Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com