Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

ANUSURIKA KUFA BAADA YA KUNG'OLEWA JINO NA KUTOBOLEWA JICHO NA MUMEWE TUHUMA ZA KUCHEPUKA NA MGENI




Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha, Justin Masejo amesema wanamtafuta Isaack Mnyagi mkazi wa Sombetini jijini  Arusha anayetuhumiwa kumpiga mwenza wake, Jackline Mnkonyi (38) na kisha kumng’oa jino la mbele na kumtoboa jicho.

Tukio hilo limetokea juzi Alhamisi Mei 25, 2023 baada ya kutokea ugomvi ambao unadaiwa kuchangiwa na wivu wa mapenzi baina ya wenza hao

Jackline ambaye ana mtoto mchanga amesema amepigwa na mumewe baada ya kumtuhumu kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mgeni aliyefika nyumbani bila kujua kama ni mjomba wake.

"Nilijitahidi sana kujieleza lakini ilishindikana alianza kunipiga kwa mateke na ngumi na alichukua Praizi na kuniamuru nifungue mdomo na kuning’oa jino moja ambapo damu zilianza kuchuruzika,”amesimulia kwa uchungu huku akilia.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com