Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

TRENI YAUA WATU WAWILI MORO


Watu wawili wamefariki Dunia baada ya kugonga Treni kwenye makutano ya reli ya mwendo kasi (SGR) na reli ya kati mtaa wa Misongeni Kata Bigwa Manispaa ya Morogoro.

Kaimu afisa Uhusiano Hospital ya rufaa mkoa wa Morogoro Scholastic Ndunga amethibitisha kupokea miili ya watu wa wili waliotambulika kwa majina ya Mussa Jackson na Ellyson Kalugadi wote wakiwa na umri wa miaka 35.

Ajali hiyo imetokea majira ya saa 3 asubuhi ambapo mashuhuda wa eneo hilo wanasema chanzo cha ajali ni vijana hao kuendesha pikipiki bila ya kufuata sheria za barabarani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com