Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

HALMASHAURI YA MANISPAA YA SHINYANGA, ICS WATOA MAFUNZO YA KUJENGA MAZINGIRA SALAMA KWA WATOTO NDANI NA NJE YA SHULE

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Halmashauri ya Manispaa ya Shinyanga kwa kushirikiana na Shirika la Investing in Children and Societies (ICS) wameendesha mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga.

Mafunzo hayo ya kujenga mazingira salama kwa watoto ndani na nje ya shule kwa watumishi na watoto Manispaa ya Shinyanga yanafanyika kuanzia leo Jumanne Mei 16,2023 hadi Mei 17,2023 katika ukumbi wa shule ya Msingi Buhangija Mjini Shinyanga.

Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko amesema mafunzo hayo yataonesha njia salama katika kuhakikisha watoto wanakuwa salama wakiwa ndani na nje ya shule.

Ameeleza kuwa, licha ya walimu kufanya kazi kubwa ya kulea watoto shuleni changamoto kubwa ipo ndani ya familia kwani wazazi na walezi wamesahau wajibu wa kulinda watoto wao hali inayochangia mmomonyoko wa maadili na kuwepo kwa vitendo vya ukatili wa kijinsia.

“Siku hizi tumekuwa na watoto wasio na adabu, vijana wasio na adabu lakini pia wazee wasio na adabu kutokana na mambo kadhaa ukiwemo utandawazi. Unakuta wazazi hawaelewani, wanagombana mbele ya watoto, hali hii inasababisha watoto wetu waige tabia za ajabu , wasiwe salama. Nidhamu ya watoto inatakiwa ianzie ndani ya familia ili kuhakikisha watoto wanakuwa salama muda wote”,ameeleza Masumbuko.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko.

Meya huyo ametumia fursa hiyo kuwakumbusha wazazi na walezi juu ya umuhimu wa kuwaeleza watoto wazi wazi madhara ya mambo yanayotokea lakini pia kuwashauri wananchi kwenda kwenye nyumba za ibada ili wawe na hofu ya Mungu kwa ajili ya kuepukana na uovu katika jamii.

“Tuwe wabunifu ili watoto wetu wawe salama, tuwe wawazi tuwaeleze watoto ukweli kuhusu madhara ya matendo ya hovyo. Tuhakikishe tunasimamia mafundisho sahihi na maadili mema ili watoto wetu wawe salama na jamii iepukane na vitendo vya ukatili wa kijinsia na maovu kama vile ushoga na usagaji”,amesema Masumbuko.

Aidha amesisitiza juu ya umuhimu wa kutoa taarifa kuhusu vitendo vya ukatili ili jamii iwe salama.

“Kama unaona kuna tukio siyo la kawaida popote pale toa taarifa. Wafundisheni watoto kutoa taarifa, ukatili na uhalifu utaisha tukitoa taarifa. Toa taarifa badala ya kunyamaza na kusema hayakuhusu. Nanyi walezi myaishi hayo mnayoyafundisha”,ameongeza Masumbuko.
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Manispaa ya Shinyanga, Sifa Amon.

Kwa upande wake, Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Divisheni ya Sekondari Manispaa ya Shinyanga, Beatrice Mbonea amesema walimu wameachiwa mzigo wa kulea watoto, wanaelemewa hivyo kuwaomba wazazi kutenga muda wa kukaa na kuzungumza na watoto wao ili kubaini changamoto zinazowakabili na mabadiliko ya watoto.

“Watoto wengi wanakuwa katika mazingira hatarishi kutokana na wazazi kuwa na shughuli nyingi ‘Busy’, kutojali na kutotenga muda wa kuongea na watoto. Walimu ni wachache wameachiwa mzigo wa kulea wanafunzi wengi, wanaelemewa. Hivyo wazazi wanatakiwa kushirikiana na walimu na majirani kulea watoto lakini ni lazima wazazi wajitahidi kuwajua marafiki wa watoto wao”,amesema Mbonea.

“Tuendelee pia kuhamasishana kuhusu kujenga hosteli kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari ili kuepusha na vishawishi wanavyokutana navyo watoto wawapo njiani kwenda au kutoka shuleni”, amesema.

Mbonea pia amewataka viongozi wa serikali za mitaa wawajibike kuangalia majengo ambayo hayatumiki/hayajakamilika kwani yamekuwa yakitumiwa na watoto na watu wazima kufanya vitendo viovu.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Shinyanga, Aisha Omary akitoa mada ya masuala ya ukatili wakati wa mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule.

Naye Meneja Miradi wa Shirika la ICS, bi. Sabrina Majikata amewahamasisha wazazi na walezi kujenga ukaribu na watoto wao ili kubaini mabadiliko ya tabia na kupata taarifa za changamoto wanazokabiliana nazo.

“ICS inajishughulisha na masuala ya kuboresha malezi na makuzi bora ya watoto na kuwaimarishia ulinzi na usalama, kuimarisha uchumi wa kaya, masuala ya UKIMWI kwa vijana na afya ya uzazi. Ili watoto wetu wawe salama tusiwaachie walimu pekee kazi ya kulea watoto kwani watoto ni wengi na walimu ni wachache, wazazi tutimize wajibu wetu”,amesema.

Kwa upande wake, Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Manispaa ya Shinyanga, Sifa Amon amesema mafunzo hayo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga yatahusisha mada mbalimbali ikiwemo masuala ya ukatili na ukatili wa kijinsia,mbinu za kulinda motto, wajibu na majukumu ya walimu wa malezi na mfumo wa utoaji taarifa.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga leo Jumanne Mei 16,2023. Picha na Kadama Malunde -Malunde 1 blog
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Ramadhan Masumbuko akizungumza wakati akifungua mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga

Naibu Mstahiki Meya Manispaa ya Shinyanga Mhe. Esther Makune akizungumza wakati wa mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga
Afisa Maendeleo ya Jamii kutoka Manispaa ya Shinyanga, Sifa Amon akizungumza wakati wa mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga
Meneja Miradi wa Shirika la ICS, bi. Sabrina Majikata akizungumza wakati wa mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga

Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Divisheni ya Sekondari Manispaa ya Shinyanga, Beatrice Mbonea akiwa kwenye mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga
Afisa Elimu ya Watu Wazima na Elimu Nje ya Mfumo Rasmi Divisheni ya Msingi Manispaa ya Shinyanga, Judith Kagembe akizungumza kwenye mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga
Mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule yakiendelea
Mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule yakiendelea
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Shinyanga, Aisha Omary akitoa mada ya masuala ya ukatili wakati wa mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga

Mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule kwa walimu wa malezi, maafisa maendeleo ya jamii na Baraza la Watoto Manispaa ya Shinyanga yakiendelea

Mafunzo ya kujenga mazingira salama ya watoto ndani na nje ya shule yakiendelea.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com