Mitumbwi
Wavuvi watatu wamefariki dunia na wengine watatu wamenusurika kifo baada ya mtumbwi waliokuwa wakiutumia kuvulia samaki kuingiliwa maji na kuzama usiku wa kuamkia Mei 8, 2023.
Mkuu wa kituo cha Zimamoto na Uokoaji mkoa wa Geita, Wambura Fidel, amesema mtumbwi huo ulikuwa na wavuvi sita lakini wakati wanaingia majini hawakuchukua tahadhari ya kuvaa vifaa vya kujiokoa.
Akiongea mara baada ya kufanya uokozi wa miili ya waliokufa maji, Mkuu wa wilaya ya Geita Cornel Magembe amewataka watu wote wanaojihusisha na shughuli za uvuvi kuhakikisha wana vifaa vya tahadhari ili inapotokea ajali waweze kuokolewa kirahisi.
Chanzo - EATV
Social Plugin