NA EMMANUEL MBATILO
KLABU ya Yanga imefanikiwa kuondoka na ushindi mnono wa mabao 2-0 dhidi ya timu ya Marumo Gallants ya nchini South Afrika katika mchezo wa mkondo wa kwanza nusu fainali Kombe la Shirikisho barani Afrika.
Katika mchezo huo ambao ulipigwa kwenye dimba la Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Yanga Sc kipindi cha kwanza walicheza kandanda safi na kupata nafasi nyingi ambazo walishindwa kuzitumia vizuri.
Kipindi cha pili Marumo Gallants walirudi wakiwa wanatawala mchezo huku wakitengeneza nafasi nyingi lakini walinzi wa Yanga walikuwa makini kuzuia mashambulizi.
Aziz Ki alianza kuitanguliza Yanga Sc mbele baada ya kufunga bao zuri akipokea pasi kutoka kwa Tusila Kisinda kabla ya Benard Morrison kufunga bao la ushindi na kuwafanya kuondoka na ushindi mnono wa mabao 2-0.
Social Plugin