BAISKELI ZA UMEME, PIKIPIKI ZITAZUIA UCHAFUZI WA MAZINGIRA NA PUNGUZA GHARAMA ZA USAFIRI
Wednesday, May 10, 2023
Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein kushoto akifuatilia vijana hao wakiendelea na utengenezaji wa pikipiki zinazotumia umeme
Vijana wakiendelea na utengenezaji wa pikipiki za umeme kama wanavyoonekana katika Shule ya Ufundi Tanga School
Vijana wakiendelea na matengenezo ya pikipiki zinazotumia umeme
Matengenezo ya Pikipi za kutumia Umeme yakiendeleaMkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maendeleo ya mafunzo hayo
Na Mwandishi Wetu,Tanga
VIJANA wanaopata mafunzo ya kutengeneza na kuunda Pikipiki na Baiskeli zinazotumia umeme Jijini Tanga wamesema kwamba zitasaidia kuzuia uchafu wa mazingira katika maeneo mbalimbali nchini. Pia, ma dereva haswa bodaboda wataweza kujiongezea kipato kwa kupunguza gharama ya mafuta na usafiri
Mafunzo hayo yanaendeshwa na Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization(TOIO) na Robotech Labs chini ya ufadhili wa Shirika la Botnar Fondation ambao wamedhamiria kutoa ujuzi kwa vijana ili kuweza kuutumia na kuweza kujikwamua kiuchumi
Akizungumza wakati mafunzo hayo yakiendelea ,Mwanafunzi wa kidato cha Pili wa shule ya Sekondari Tanga Ufundi Saidi Kasim alisema mafunzo hayo yanawapa mwanga mzuri wa mbeleni kutokana na kwamba ujuzi wanaoupata utawasaidia kuweza kujiajiri
Alisema kutokana na kwamba mbinu mbalimbali ambazo wamekuwa wakifundishwa siku hadi siku ikiwemo jinsi ya kutenegenza pikipiki za umeme na baiskeli kutokana kwa mkufunzi wao na hivyo kuwa njia nzuri ya kuweza kukabiliana na soko la ajira hapa nchini.
Aidha alisema kutokana na kwamba hivi sasa zipo changamoto mbalimbali zinazotokana na uchafuzi wa mazingira na hivyo wakati Serikali ikichukua jitihada za kukabiliana nayo mradi huo utakuwa ni wa manufaa kutokana na kujibu tatizo hilo.
“Mafunzo haya na pikipiki za umeme na baiskeli tunayojifunza hapa ni jinsi zinavyotengenezwa na namna ya kuweka fremu zanje na kuweka waya hakika mradi huu utatusaidia sana “Alisema
“Lakini pia utatusaidia kujiajiri pindi tunapomaliza shule na kwenda nje tunaweza kuanzisha mradi wa kubadilisha pikipiki za kawaida na zikawa zinatumia umeme kutokana na kwamba sio jambo gumu”Alisema
Haya hivyo alitoa wito kwa vijana wengine Jijini Tanga kuchangamkia mafunzo hayo kutokana na umuhimu wake wa kuweza kuwaandaa kujiajiri baadae na hivyo kujikwamua kiuchumi wao na jamii zao
Naye kwa upande wake Peter Sanga ambaye ni mwanafunzi wa kidato cha pili alisema mafunzo ambayo wamefundishwa kwenye mradi huo yamewawezesha kufahamu namna ya kuzibadilisha pikipiki za umeme na baiskeli kutoka zilivyokuwa awali zikitumia mafuta.
Hata hivyo alisema pia wamefundishwa namna ya kutengeneza pikipiki na baiskeli hizo kutumia umeme na hilo ni jambo muhimu kutokana na kwamba kipindi hiki uchafuzi wa mazingira umekuwa mkubwa sana.
“Kwa sababu ukifuatilia vyombo vingi vya usafiri vimekuwa vikitumia mafuta na yamekuwa ni chanzo cha kuchafua mazingira hivyo vyombo hivyo ni muhimu kwa lengo la kutunza mazingira”Alisema
Aliongeza kwamba mradi huo una umuhimu mkubwa katika kutunza mazingira kwa sababu vitakapokuwepo hata vyombo vinavyotumia mafuta vitapungua na hivyo kuwa moja ya kutunza mazingira.
Awali akizungumza Mkurugenzi wa Taasisi ya Tanzania Open Innovation Organization (TOIO) Shaukatali Hussein alisema kwamba wameanza fursa ya mafunzo hayo kuanzia May 5 -10 kuhusu pikipiki na baiskeli za umeme lengo wanataka vijana kutoka kata mbalimbali wachangamkie fursa ya kusoma jinsi ya kuviunga,kuvirekebisha na kutenegenza baiskeli na pikipiki za umeme.
Alisema somo hilo lina vipindi viwili awamu ya kwanza ni kuanzia asubuhi saa nne mpaka saa sita na pili kuanzia saa nane mpaka saa kumi mpaka sasa wamepata vijana zaidi ya 30 huku akitoa shukrani za dhati kwa Jiji la Tanga na Taasisi ya Fondation Botnar ambao wamewezesha kutoa mafunzo hayo kwa vijana mbalimbali.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin