Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

AMUUA MKE MWENZA KWA KUMCHOMA SINDANO YA SUMU


Maafisa wa Polisi nchini Uganda wanamsaka mwanamke anayedaiwa kutoroka nyumbani baada ya kumchoma mke mwenza kwa sindano iliyokuwa na sumu.

Jackie Namubiru anadaiwa kumuua mke mwenza Nakimera Lydia mwenye umri wa miaka 23, baada ya kumdunga sindano yenye sumu na kutoroka. 

Kwa mujibu wa ripoti iliyochapishwa na jarida la Nilepost, Lydia alikimbizwa katika Kliniki ya Bulamu na kuhamishwa hadi Hospitali ya Byansi iliyoko Masaka baada ya hali yake kuzidi kuwa mbaya.

"Mwathiriwa aliaga dunia kwa kutiliwa sumu mwilini mnamo Aprili 24, 2023 saa kumi na mbili  na nusu jioni,” msemaji wa polisi Fred Enanga alisema siku ya Jumanne.

Enanga aliongeza kusema kwamba tukio hilo huenda lilitendeka kutokana na wivu baina ya wake wenza hao na kwa sasa mshukiwa anasakwa vikali na maafisa wa polisi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com