Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Wadau wa Lishe Mkoa wa Shinyanga wamefanya kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi katika shule na jamii kwa ujumla unaosimamiwa na kutekelezwa kwa ushirikiano baina ya Serikali na Shirika lisilo la Kiserikali Global Alliance for Improved Nutrition - GAIN pamoja na Kampuni ya SANKU Project Healthy Children Ltd.
Akizungumza wakati wa kikao hicho leo Ijumaa Mei 19,2023 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo amesema lishe bora katika jamii ni kichocheo cha maendeleo katika nyanja zote (Afya, Kilimo, Elimu, Biashara, Uchumi, nk).
Amesema ni pale tu ambapo athari za lishe duni au utapiamlo zitakapodhibitiwa au kutokomezwa ndipo malengo ya maendeleo katika nyanja hizo yataweza kufikiwa kwa ufanisi.
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akifungua kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni.
“Jambo la msingi ambalo sote tunapaswa kulifahamu na kuzingatia ni ukweli kwamba lishe ni suala mtambuka na utapiamlo katika jamii ni matokeo ya mkusanyiko wa matatizo mengi. Matatizo hayo yanaweza kusababishwa na Ulaji duni na Mtindo wa Maisha usiofaa, Maradhi mbalimbali, kutokuwa na Uhakika wa Chakula, Matunzo duni ya Mama na Mtoto, Mazingira Machafu, Rasilimali haba na mgawanyo wa rasilimali usiokuwa na uwiano sahihi kijinsia, Umaskini wa kipato, machafuko ya kisiasa na hata sera zisizotambua umuhimu wa lishe kwa maendeleo ya mwanadamu na taifa kwa ujumla”,amesema Chambi.
Ameeleza kuwa Utapiamlo ni tatizo kubwa linaloathiri afya hasa ya watoto chini ya miaka mitano na Wanawake walio katika umri wa kuzaa.
“Takwimu za afya za kitaifa za hivi karibuni (TDHS 2022) zimebaini kuwa Mkoa wa Shinyanga una asilimia 27.5 ya watoto waliodumaa. Hii ndio sababu kubwa iliyotufanya kuwatafuta wenzetu GAIN na SANKU ili tuweze kushirikiana katika kutatua moja ya visababishi wa kiwango hiki cha udumavu katika Mkoa wa Shinyanga ambapo itasaidia kupatikana chakula kilichoongezewa Virutubishi”,amesema Katibu Tawala huyo.
Wadau wa Lishe wakiwa ukumbini
Amesema Mradi huo wa uhamasishaji na ulaji wa vyakula vilivyoongezewa virutubishi ni fursa kwa mkoa wa Shinyanga hivyo viongozi na watendaji wa ngazi mbalimbali watoe ushirikiano wa kutosha ili utekelezaji wa mradi ufikie malengo yaliyokusudiwa ikiwa ni pamoja na kuimarika kwa afya na lishe ya jamii ambayo ni mtaji mkubwa na nguvu kazi ya Taifa.
Aidha ameziagiza Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wadau kwa pamoja kuendelea kuelimisha jamii kuhusu faida ya kuongeza virutubishi katika vyakula ili jamii iweze kutumia vyakula hivyo kwa kutumia waandishi wa habari katika maeneo yao.
“Ikumbukwe kuwa; mnamo tarehe 30 Septemba, 2022, wakati wa kusaini Mkataba wa usimamiaji masuala ya lishe, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alituelekeza kuendelea kuongeza juhudi za kuhakikisha tunapunguza kiwango kikubwa cha udumavu na athari zake hapa nchini”,amesema Chambi.
“Tutaendelea kusimamia utekelezaji wa Mkataba huu ili ulete tija katika jamii zetu na Mradi huu unakwenda kutekeleza kiashiria kimojawapo kilichopo kwenye Mkataba huu. Nitumie fursa hii kuwaalika Wadau wengine wanaoweza kuja na miradi yenye ubunifu wa kusaidia kupunguza udumavu kwa watoto chini ya Miaka mitano ili tujenge kizazi chenye ubora wa kuleta maendeleo kwa miaka ya usoni”,ameongeza Chambi.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu amevitaja virutubishi vinavyoongezwa kwenye vyakula ni Madini Chuma (Iron) kwa ajili ya kuongeza damu, Madini ya Zinki kuimarisha Kinga ya mwili na uimara wa mishipa ya damu, Vitamini A na Foliki Asidi (Folic Acid) kwa ajili ya kusaidia uumbaji wa mtoto.
Naye Afisa Lishe kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI, Mariam Nakuwa amesema Programu ya kuongeza upatikanaji na matumizi ya vyakula vilivyorutubishwa shuleni ni sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan ili kupunguza changamoto za lishe duni na kuboresha elimu ya msingi na sekondari.
Akitoa maelekezo kwa niaba ya Ofisi ya Rais TAMISEMI ,Nakuwa amesema :
“Vyakula vinavyoliwa katika shule zote za msingi na Sekondari viwe ni vile vilivyoongezewa virutubishi kwa mujibu wa sheria na miongozo iliyopo, Wazabuni wote wanaolisha shule wanazingatia na kuleta vyakula vilivyoongezewa virutubishi (Fortified foods) katika shule wanakolisha, Taasisi zote zinazohusika na udhibiti ubora na kuhakikisha usalama wa chakula vihakikishe vinafanya ufuatiliahji na usimamizi wa karibu ili kuepuka madhara yanayoweza kutokea kama taratibu hazitazingatiwa”.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Dedan Rutazika amesema watahakikisha kila shule inapata vyakula vyenye lishe ili kupunguza changamoto ya udumavu na upungufu wa damu na changamoto zingine zinazotokana na lishe.
Meneja Mwandamizi wa Kampuni ya SANKU inayojihusisha na urutubishaji wa unga wa mahindi nchini Tanzania, bw. Gwao Omary amesema hivi sasa wanafanya kazi na wazalishaji 726 wa mahindi na wamefunga vinu vya kuongeza virutubishi 837 nchi nzima wanaendelea kushirikiana na serikali ili kuhakikisha watoto wanapata lishe shuleni.
Meneja wa Mradi wa Urutubishaji chakula Shirika la GAIN Tanzania, Archard Ngemela amesema mradi huo unaotekelezwa katika mikoa yote ya Kanda ya ziwa ukilenga shule moja kwa moja shule 40 kila mkoa unatarajiwa kuona viashiria vya utapiamlo vinapungua hususan udumavu kwa watoto chini ya miaka mitano na tatizo la upungufu wa damu kwa vijana balehe na akina mama litapungua au kuisha kabisa.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akifungua kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo leo Ijumaa Mei 19,2023. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Katibu Tawala Wilaya ya Shinyanga, Boniphace Chambi akifungua kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni kwa niaba ya Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga Prof. Siza Tumbo leo Ijumaa Mei 19,2023.

Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Rad. Faustine Mulyutu akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Dedan Rutazika akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni.
Kaimu Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga, Dedan Rutazika akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni.
Afisa Lishe OR – TAMISEMI, Mariam Nakuwa akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni.
Afisa Lishe OR – TAMISEMI, Mariam Nakuwa akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Afisa Lishe OR – TAMISEMI, Mariam Nakuwa akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Meneja Mwandamizi wa Kampuni ya SANKU akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Meneja Mwandamizi wa Kampuni ya SANKU akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Meneja wa Mradi wa Urutubishaji chakula Shirika la GAIN Tanzania, Archard Ngemela akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni

Afisa Lishe Mkoa wa Shinyanga Yusuph Hamis akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Afisa Lishe Mkoa wa Shinyanga Yusuph Hamis akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Afisa Lishe Mwandamizi kutoa Wizara ya Afya, Peter Francis Kaja akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Meneja Kanda ya Ziwa Kampuni ya Sanku Erasmus Minja akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Afisa Habari na Mawasiliano Shirika la Child Help Tanzania, Milton Byemerwa akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Afisa Lishe Mtafiti kutoka taasisi ya Chakula na Lishe (TFNC) , Doris Katana akizungumza kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Wadau wakiwa kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni

Wadau wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Wadau wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni
Wadau wakipiga picha ya kumbukumbu kwenye kikao cha kuanza kwa mradi wa kuongeza upatikanaji na matumizi ya Vyakula vilivyoongezwa virutubishi shuleni.
Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin