Afisa mahusiano kazini wa mgodi wa Barrick North Mara, Daniel John Paul,akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakati wa kongamano la kuwajengea uwezo lililoandaliwa na taasisi ya AIESEC Tanzania kwa udhamini wa kampuni ya Barrick na kufanyika chuoni hapo mwishoni mwa wiki.
Mwakilishi wa Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa Taaluma ,utafiti na ushauri ,Afisa Mahusiano na Masoko wa Chuo Kikuu cha Iringa Crispin Nyomoye,akifungua kongamano hilo.
Afisa Rasilimali watu wa Barrick North Mara Innocent Kishobera, akiongea na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakati wa kongamano
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zinatolewa wakati wa kongamano hilo.
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa wakiwa wameshika vipeperushi vya kampuni ya Barrick ambayo imedhamini kongamano hilo.
Maofisa wa Barrick katika picha ya pamoja na viongozi wa AIESEC Tanzania na Mwakilishi wa Mgeni Rasmi,Crispin Nyomoye
*****
Kampuni ya Barrick Gold Corporation, imedhamini na kushiriki katika kongamano la wanafunzi wa vyuo vikuu lililoandaliwa na taasisi ya kuchipua na kuendeleza vipaji vya uongozi kwa vijana (AIESEC Tanzania) lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Iringa na kuwashirikisha wanafunzi,wahadhiri na wadau mbalimbali.
Kupitia kongamano hili ambalo hufanyika kila mwaka, wanafunzi huweza kufahamu jinsi taasisi mbalimbali nchini zinavyoendesha shughuli zake lengo kubwa ikiwa ni kuwajengea uwezo wa kujua vipaji walivyonavyo, kujifunza jinsi ya kujiamini na kukabiliana na ushindani katika soko la ajira, kujitambua uwezo wao ni jinsi gani wanaweza kushiriki kutoa mchango wa kuendeleza taifa pindi wamalizapo masomo yao.
Maofisa Raslimali Watu Waandamizi wa Barrick pia walishiriki katika maonesho na kongamano hilo ambapo walipata fursa kuzungumza na wanafunzi kuhusiana na kukabiliana na changamoto mbalimbali ikiwemo ajira,kuendeleza vipaji vyao pia wanafunzi walipata fursa kuelewa jinsi kampuni ya kimataifa ya Barrick, inavyoendesha shuguli zake kwa kutoa kipaumbele kusaidia jamii sambamba na mpango wake wa kuibua na ukuzaji wa vipaji kwa vijana wa kitanzania na wafanyakazi wake.
Social Plugin