Na. Mwandishi wetu Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi mkoani Arusha Mei 27, 2023 limefanikiwa kumtamata mtuhumiwa aitwaye Isack Robertson (45) mkazi wa Sombetini Jijini Arusha kwa tuhuma za kumpiga na kumjeruhi mke wake aitwaye Jackline Mkonyi (38) mkazi wa Sombetini jijini humo.
Akitoa taarifa hiyo Mei 28, 2023 Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Justine Masejo amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa huko katika maeneo ya Himo mkoani Kilimanjaro na wanaendelea kumhoji na pindi upelelezi utakapokamilika jalada litapelekwa ofisi ya Taifa ya Mashtaka kwa hatua zaidi za kisheria.
Aidha ametoa onyo kwa baadhi ya watu wachache wanaofanya vitendo vya ukatili katika familia zao ama sehemu nyingine kuacha mara moja kwani hawatasita kuwakamata na kuwachukulia hatua za kisheria.
Social Plugin