Na Kadama Malunde – Malunde 1 blog
Ukarabati na Upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga umeanza ukitarajiwa kurahisisha usafiri kwa wananchi pamoja na kuchochea ukuaji wa uchumi hususani katika sekta ya madini mkoani na taifa kwa ujumla.
Akizungumza leo Mei 30,2023, Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme kwenye Mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS uliofanyika katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga amesema ni muhimu ujenzi wa uwanja wa Ndege Shinyanga uzingatie viwango vinavyotakiwa kulingana na thamani ya pesa na ukamilike ndani ya wakati.
“Tunamshukuru sana Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutuletea fedha kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege. Kwa muda mrefu watu wa Shinyanga wamekuwa na shauku kubwa ya kupata uwanja wa ndege kwani wamekuwa wakilazimika kusafiri kwenda mkoani Mwanza kupanda ndege umbali wa kilomita 164”,amesema Samizi.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati Wadau wa Usafiri wa Anga wakitembelea uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
“Tumekutana hapa kwa ajili ya mkutano wa wadau wa usafiri wa anga lakini pia mkutano huu tuutumie kama uzinduzi rasmi wa ujenzi wa mradi huu. Rai yangu kwa wananchi wa Shinyanga ni kuchangamkia fursa kupitia mradi huu, tengenezeni shughuli ambazo zitachochea uchumi na tuhakikishe tunaulinda mradi huu”,ameongeza Samizi.
Akielezea kuhusu ujenzi huo, Meneja Miradi Viwanja vya ndege - TANROADS kutoka makao makuu Mhandisi Neema Joseph amesema mradi wa Ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Shinyanga unajengwa na Mkandarasi China Hennan International Corperation Group Co. Ltd (CHICO) kwa gharama ya shilingi 49,179,439,633.00/= pamoja na VAT na unasimamiwa na Wakandarasi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia kwa gharama ya Dola za Marekani 2,602,343 na Shilingi 23,735,554/= pamoja na VAT.
Mhandisi Neema amesema mradi huo ambao ujenzi wake umeanza Aprili 4,2023 unatarajia kukamilika ifikapo Oktoba 3,2024 (ndani miezi 18) kwa ufadhili wa Benki ya Uwekezaji ya Ulaya (EIB).
“Kazi zikatazofanyika ni ukarabati wa barabara ya kutua na kurukia ndege (Runway) kwa kiwango cha lami, ukarabati wa barabara ya kiungio na maegesho ya ndege kwa kiwango cha lami, ujenzi wa jingo la abiria pamoja na ATC na huduma za hali ya hewa, ujenzi wa barabara ya kuingia uwanjani”,amesema Mhandisi Neema.
Amezitaja kazi zingine kuwa ni ujenzi wa maegesho ya magari, ujenzi wa uzio wa usalama, ununuzi na usimikaji wat aa za kuongozea ndege (AGL), ununuzi na usimikaji wa mitambo ya usalama (DVOR/DME) na ujenzi wa kituo cha umeme (energy centre).
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi amewataka wakazi wa Shinyanga kulinda mradi huo na kuepuka vitendo vya kuhujumu kama vile wizi wa mafuta na vifaa vingine vya ujenzi huku akisisitiza kuwa mradi huo utawanufaisha wananchi wa maeneo ya karibu kupata ajira ya muda na kupata fursa mbalimbali za kiuchumi.
“Tunawahakikishia kuwa ujenzi wa mradi tutausimamia kwa viwango vinavyotakiwa kwa kuzingatia thamani ya pesa iliyotolewa. Naomba tushirikiane. Wananchi tuwe walinzi wa mali za mkandarasi na tutoe taarifa kama mnaona kuna mtu anataka kuhujumu mradi huu”,amesema Ndirimbi.
Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma za ufundi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Dk. Pascal Waniha amemshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za ujenzi wa mradi huo.
Nao wadau wa usafiri wa anga akiwemo Mchungaji Greyson Kinyaha kutoka kanisa la KKKT Dayosisi Kusini Mashariki mwa Ziwa Victoria, Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana na Catherine Mlandaja kutoka Mgodi wa Williamson Diamonds wamesema muda uliopangwa ni mwingi hivyo wajaribu kuharakisha ili kuweza kukamilisha kabla ya mikataba ulivyopangwa kwani shauku kubwa ya wana Shinyanga ni kuona uwanja wa ndege unatumika.
ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa. Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa. Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli.
Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa katika uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga leo Jumanne Mei 30,2023 wakati wa Mkutano wa wadau wa usafiri wa anga ulioenda sanjari na uzinduzi wa ujenzi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli.

Msimamizi wa mradi wa ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga Mhandisi Donatus Binemungu akiwaelezea Wadau wa Usafiri wa Anga ujenzi wa uwanja wa Ndege wa Ibadakuli Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati Wadau wa Usafiri wa Anga wakitembelea uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia, Nasser Elgohary akimuonesha Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi ramani ya ujenzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga.
Mhandisi Mkazi kutoka Kampuni ya SMEC International ya nchini Australia, Nasser Elgohary akionesha ramani ya ujenzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga.

Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa uwanja wa Ndege Shinyanga kutoka TANROADS, Donatus Binemungu akielezea kuhusu ramani ya ujenzi wa uwanja wa ndege Ibadakuli Shinyanga.
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga Mhe. Johari Samizi akizungumza kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Meneja Miradi Viwanja vya ndege - TANROADS kutoka makao makuu Mhandisi Neema Joseph akitoa taarifa ya upanuzi na ukarabati wa uwanja wa Ndege Shinyanga wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Meneja Miradi Viwanja vya ndege- TANROADS kutoka makao makuu Mhandisi Neema Joseph akitoa taarifa ya upanuzi na ukarabati wa uwanja wa Ndege Shinyanga wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Meneja wa TANROADS Mkoa wa Shinyanga, Mhandisi Mibara Ndirimbi akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Katibu wa CCM Wilaya ya Kishapu, Peter Mashenji akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mhandisi wa Mradi wa Ujenzi wa uwanja wa Ndege Shinyanga kutoka TANROADS, Donatus Binemungu akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Meneja wa Benki ya CRDB Kanda ya Magharibi Jumanne Wagana akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mganga Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Yudas Ndungile akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mdau wa usafiri wa anga Catherine Mlandaja kutoka Mgodi wa Williamson Diamonds akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mkurugenzi wa Miundombinu na Huduma za ufundi kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa (TMA) Dk. Pascal Waniha akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.
Mdau wa usafiri wa anga akizungumza wakati wa mkutano wa Wadau wa Usafiri wa Anga na TANROADS katika uwanja wa Ndege wa Shinyanga.

Wadau wa Usafiri wa Anga wakiwa kwenye mkutano.

Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Social Plugin