Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya Nyangoto kilichopo Kata ya Nyamongo, Tarime Vijijini, Dk Isack Sima ameuawa kwa kukatwakatwa mapanga na watu wasiojulikana wakati akitoka kituo chake cha kazi usiku akirejea nyumbani.
Dk. Sima ambaye inadaiwa aliuawa Mei 3 zilizopita, taarifa zilizosambaa mitandaoni leo Mei 6, 2023 zimeeleza kuwa juzi alishinda kazini akihudumia wagonjwa hadi usiku.
“Ni kawaida yake kujitoa hata muda wa ziada. Wakati anarudi nyumbani, alikutana na watu waliosimamisha pikipiki yake na kumshambulia kwa mapanga. Amekatwa kichwani, mgongoni, mikononi, miguuni yani hata haielezeki. Ameuawa kinyama,” kilieleza chanzo hicho.
Social Plugin