Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

PJFC NA ISAMILO JOGGING WAENDESHA BONANZA LA MICHEZO SHINYANGA, KAMANDA MAGOMI AKEMEA VITENDO VYA UKATILI


Na Mwandishi wetu - Malunde 1 blog
Kikundi cha Mazoezi mkoani Shinyanga maarufu Polisi Jamii Fitness Center (PJFC) na Isamilo Jogging wameendesha Bonanza la Michezo Mjini Shinyanga.


Bonanza hilo la michezo limefanyika leo Mei 20 ,2023 kwenye viwanja vya michezo vya chuo cha ualimu Shinyanga (SHY COM), kwa kucheza mpira wa miguu, kati ya timu ya Isamilo Jogging kutoka Jijini Mwanza na Polisi Jamii Fitness Center kutoa mkoani Shinyanga .

Akizungumza kwenye Bonanza hilo Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amezitaka Klabu zinazofanya mazoezi mkoani humo kuendelea kupinga vitendo vya ukatili na uhalifu katika maeneo yao ya mazoezi.

Kamanda Magomi amesema kuwa iwapo jamii itashirikiana na jeshi la polisi katika mapambano ya kupinga vitendo vya ukatili na uhalifu
itasaidia mkoa wa Shinyanga na Taifa kuwa salama.

“Bonanza hili limeshirikisha timu ya PJFC kutoka Shinyanga na Timu ya Isamilo Jogging kutoka mkoani Mwanza na jeshi la polisi ili
kuwauganisha kuwa kitu kimoja katika Mapambano dhidi ya vitendo vya uhalifu na ukatili ndani ya mkoa huo,”amesema Magomi.

Naye Mwenyekiti wa Clabu ya Mazoezi PJFC mkoa wa Shinyanga Sadick Kibila, amempongeza kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi kwa kujitoa kukilea kikundi hicho na kushiriki katika mazoezi hali ambayo inawapa motisha ya kuendelea kufanya mazoezi na kushiriki katika mapambano ya kupinga vitendo vya ukatili na uhalifu mkoani humo.

Pia Kibila amewashukuru Isamilo Jogging Club kutoka mkoani Mwanza kwa kufika mkoani humo na kushirikiana nao wakati wa kufanya mazoezi ya pamoja katika uwanja wa chuo cha ualimu Shinyanga (Shy Com).

Kwa`upande wake mwenyekiti wa Isamilo Jogging Club Abdulrazak Twaha amewashukuru Clabu ya Mazoezi PJFC kwa mapokezi na ushirikiano mzuri waliouonyesha wakati wa mapokezi yao.
Picha ya pamoja ACP Janeth Magomi na Timu za mpira wa miguu Isamilo Jogging Club na PJFC
Picha ya pamoja kamanda wa polisi Shinyanga ACP. Janeth Magomi akiwa na wana Isamilo Jogging Club.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Janeth Magomi akizungumza na wana Jogging
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga ACP. Janeth Magomi kushoto akikabidhi tuzo ya pongezi kwa aliyekuwa manzilishi wa Shinyanga Madini Marathon Roland Mwalyambi ikipokelewa kwa niaba .
Mwenyekiti wa Isamilo Jogging Club Abdurazak Twaha akizungumza na wana jogging.
Timu ya mpira wa miguu PJFC.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com