WASHIRIKI kutoka Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika (EASTC) wakiwa katika picha ya pamoja kwenye banda la Chuo hicho wakati wa Maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi yanayoratibiwa na Baraza la Taifa la Elimu na Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (NACTVET) yanayoendelea viwanja vya Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha.
Na Alex Sonna-ARUSHA
CHUO cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika (EASTC) kimeshiriki Maonesho ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi- NACTVET yanayoendelea jijini Arusha.
Akizungumza kwenye banda la taasisi hiyo Mkuu wa Kitengo cha Mahusiano na Masoko Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika (EASTC), Eusebius Mwisongo,amesema kuwa maonesho hayo ni mazuri na wananchi mbalimbali wamejitokeza katika banda hilo.
''Tumefurahishwa na mwitikio mkubwa unaondelea kuoneshwa na wakazi wa Arusha wananchi mbalimbali pamoja na wanafunzi wamezidi kujitokeza katika banda letu kwa wingi lengo ni kuja kujifunza na kupatiwa elimu kuhusu kozi zinazotolewa na chuo chetu''amesema Bw.Mwisongo
Aidha Bw.Mwisongo,ametoa wito kwa wananchi kutembelea banda la Chuo hicho kwani timu nzima ya masoko ipo tayari kuwahudumia na kutoa elimu kwa undani zaidi kuhusu kozi mbalimbali zinazotolewa na chuo hicho.
Hata hivyo amewataka waendelee kutembelea website yetu ya www.eastc.ac tz ambao watapata taarifa zaidi na mawasiliano yetu kwa ufafanuzi zaidi.
Pia Mwisongo ametaja kozi wanazozitoa kuwa ni Master of Official Statistics,Master of Science in Agricultural Statistics,Postgraduate Diploma in Official Statistics,Postgraduate Diploma in Agricultural Statistics,Bachelor of Official Statistics,Bachelor Degree in Data Science, Bachelor Degree in Business Statistics and Economics, Bachelor Degree in Agriculture Statistics and Economics, Diploma in Statistics, Diploma in Information Technology,Certificate in Statistics, Certificate in Information Technology
Social Plugin