CHUO KIKUU MZUMBE CHASAINI MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA CHUO KIKUU MALAWI (UNIMA)


Chuo Kikuu Mzumbe Leo kimesaini makubaliano ya Ushirikiano na Chuo Kikuu Malawi(UNIMA), katika sherehe fupi iliyofanyika Ndaki ya Mbeya na kuhususisha Kaimu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Mzumbe, Prof. William Mwegoha na Prof. Samson Sajidu, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu Malawi (UNIMA).

Makubaliano hayo yatawezesha vyuo hivyo kuanzisha programu za mafunzo ya Pamoja, Utafiti, pamoja na kubadilishana ujuzi na wataalamu.

Akizungumza baada ya kusaini makubaliano hayo, Makamu Mkuu wa Chuo Malawi Prof. Samson amesema amefarijika sana kuona ushirikiano kati ya vyuo hivi viwili kati ya Tanzania na Malawi, unaanzishwa katika kufikia malengo mapana ya kitaaluma kwa nchi za Afrika.

Kwa upande wake Prof. Mwegoha ameahidi kuhakikisha mkataba huo unatekelezwa kwa manufaa mapana ya Taifa na Mzumbe kwa ujumla

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post