INAHITAJIKA HAMASA KWA WANAWAKE NA VIJANA KUSHIRIKI KWENYE SEKTA YA KILIMO


NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

SERIKALI pamoja na Wadau wa Kilimo nchini wameshauriwa kuweka hamasa zaidi kwenye Sekta ya Kilimo kuchochea vijana na wanawake kushiriki katika Kilimo ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kulipeleka taifa mbele kupitia sekta ya kilimo.

Akizungumza leo Mei 17,2023 katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) zinazoandaliwa na TGNP Mtandao Jijini Dar es Salaam Bw.Suleiman Omary amesema vijana wengi hawako tayari kuingia kwenye kilimo kwasababu hawajatengenezwa kisaikolojia kwamba kuona faida na kile ambacho anakifanya kwenye kilimo.

"Upatu unaopigwa kwenye masuala mengine ambayo yanawahamasisha vijana pia watumie mtindo huo huo katika kuwaelimisha vijana na kuwaonyesha faida ya kilimo na tunaweza kufika mbali kama taifa". Amesema

Kwa upande wake Mwezeshaji kutoka Jukwaa la Wadau wa Kilimo Wasio wa Kiserikali Bw. Owen Nelson amesema wanawake wamekuwa wakishiriki vizuri kwenye sekta ya kilimo ambao unaonekana katika zile shughuli zinazofanyika lakini kwenye suala la kipato wamekuwa wakiachwa nyuma kwasababu wanaume unakuta ndo wamiliki wa rasilimali.

"Wakati mwingine inakuwa ni ngumu kuweza kuona na kujua ni namna gani ambavyo wanawake wanashirikikwenye sekta ya kilimo kwasababu mwishoni kabisa mazao yanapokuwa yakiuzwa mara nyingi wanaume wanakuwa wanashirikilakini ukienda shambani ukiangalianguvu kazi kubwa inatolewa na wakina mama". Amesema


Aidha ameshauri jamii iweze kuelewa umuhimu wa ushiriki wa wanawake kwenye sekta ya kilimo na tabaka la wanaume liweze kuona wakina mama ni sehemu muhimu kuhusishwa kwenye shughuli zote za kilimo kwa kushirikiana pamoja kuanzia shambani hadi kwenye mauzo.










Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post