Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw.Kaspar Mmuya, akizungumza wakati akifungua kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw.Kaspar Mmuya,akisisitiza jambo kwa washiriki wakati akifungua kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Mkuu wa Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM)-Tanzania Bw.Maurizio, akizungumza wakati wa kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNICEF Joseph Matumbwi ,akizungumza wakati wa kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii Zanzibar Bw.Hassan Ibrahim Suleiman, akizungumza wakati wa kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella,akizungumza wakati wa kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Sehemu ya washiriki wakifatilia hotuba ya Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw.Kaspar Mmuya (hayupo pichani) wakati akifungua kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw.Kaspar Mmuya, akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kufungua kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa Mpango kazi wa kitaifa wa Kuzuia na Kupambana na Biashara Haramu ya Usafirishaji wa Binadamu kinachofanyika kwa siku mbili jijini Dodoma.
Alex Sonna-DODOMA
SERIKALI imewataka wadau na jamii kupaza sauti kuhusiana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu ili Serikali iweze kujua na kuchukua hatua kali kwa wahusika.
Hayo yameelezwa leo Mei 4,2023 jijini Dodoma na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,Bw. Kaspar Mmuya, wakati akifungua kikao cha wadau cha kufanya tathmini ya utekelezaji wa mpango kazi wa kitaifa wa kuzuia na kupambana na biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu.
Bw.Mmuya amesema Wizara yake inasimamia utekelezaji wa sheria na kila raia anapaswa azifuate ikiwa ni pamoja na kuacha biashara haramu ya kusafirisha binadamu.
“Sasa hivi kuna changamoto kubwa ya kuiga tabia, tunawachukua watu kwa upendo kumbe tunaenda kuwapeleka katika matendo ambayo sio sahihi ,hapana sio ndani ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,”amesema Bw.Mmuya
Bw.Mmuya amesema jamii inapaswa kupaza sauti kuhusiana na jambo hilo ili serikali iweze kujua na kuchukua hatua.
Amesema watunga sera na sheria ndio wasemaji wazuri wanaotetea katika ngazi ya jamii ambapo tatizo hilo lipo.
“Wale wakisimama na kulikemea kuwa hili ni tatizo tunaweza kwenda hatua nyingine,unakuta sisi wenyewe tunasema wale ambao wana platform kubwa ya kusema katika jamii hawana uelewa wa kutosha ama la,”amesema Bw.Mmuya
Hata hivyo Bw.Mmuya amesema wadau hao katika majukumu yao ni lazima waelekeze ni kazi zipi zimefanyika kwa ajili ya kuwasaidia wahanga na zimefanyika kwa kiwango gani na Je malengo yamefikiwa kwa kiwango gani.
Pia amesema mikakati au kazi zilizofanywa ili kuimarisha utaratibu na ushirikiano zimefanyika kwa kiasi gani ili wengine wajifunze.
“Msisite kueleza changamoto zipi zimejitokeza katia utekelezaji wa mpango kazi ni muhimu ila hakikisheni mnatofautisha changamoto na udhaifu,madhaifu siku zote ni malalamiko lalamiko tu”amesema Bw.Mmuya
Pia amesema kikao hicho kivumbie na kubainisha fursa zilizopo Tanzania Bara na Zanzibar.
“Niwaombe mtekeleze kazi ambazo hazijatekelezwa. Thamani ya kazi yenu kwanza ni kujikubali wewe mwenyewe kazi yako inahusiana na utu na matendo ya huruma,”amesema
Kwa upande wake Katibu wa Sekretarieti ya Kuzuia na Kupambana na Usafirishaji Haramu wa Binadamu,Seperatus Fella, amesema lengo la kikao hicho ni kupitia na kutathmini utekelezaji wa ikiwa ni pamoja na kufanya ufatiliaji ili kuona mafanikio, changamoto zilizokwamisha utekelezaji na kuweka mkakati na mpango kazi madhubuti ili kuboresha utendaji kazi.
Naye Mkurugenzi wa Ustawi wa Jamii kutoka Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Zanzibar Bw.Hassan Ibrahim Suleiman, amesema kuwa Idara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Shirika la IOM na Mashirika mengine wamekuwa wakitoa elimu kwa jamii kwa njia mbalimbali, kuwazuia katika maeneo ya Bandari kwa kupata taarifa za matukio hayo na kuwaweka katika nyumba salama kwa malazi, mavazi kuwapatia ujuzi na baadaye kuwarejesha kwao.
Awali Mwakilishi wa Shirika la Kimataifa la UNICEF Joseph Matumbwi , amesema kuwa Usafirishaji Haramu wa Binadamu ni jambo ambalo linawaathiri sana Watoto, hivyo katika utekelezaji wa mpango kazi ni vyema kuangalia yale ambayo yanawafaa katika kuhakikisha matamanio yao yanafikiwa, kuwasaidia wahanga kwa kadri ya Sheria inavyotaka, kuwafikisha katika maeneo salama na kuwarudisha katika maeneo wanapotoka.
''UNICEF itaendelea kushirikiana na Serikali ya Tanzania, Shirika la IOM kwa kufanya kazi na kuweza kuwasaidia Watoto wa Tanzania dhidi ya janga hili hata baada ya kukamilika kwa muda wa mpango.''amesema