Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena,akitoa taarifa kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu wahitimu wa kidato cha sita 2023 kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria leo Mei 25,2023 katika Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma.
Na.Alex Sonna-CHAMWINO
Jeshi la kujenga Taifa JKT limewataka wahitimu wa kidato cha sita waliohitimu elimu ya Sekondari kwa mwaka 2023 kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa Mujibu wa Sheria kwa mwaka 2023.
Akitoa taarifa kwa waandishi wa habari leo Mei 25,2023 Makao Makuu ya JKT Chamwino Dodoma Mkuu wa Tawi la Utawala JKT Brigedia Jenerali Hassan Mabena, amesema vijana hao wanatakiwa kuanza kuripoti katika makambi waliyopangiwa kuanzia June 1 hadi June 11, 2023.
Amesema JKT limewapangia makambi watakayokwenda kupatiwa mafunzo na wanatakiwa kuripoti makambini kuanzia tarehe 01 june hadi 11 June, 2023.
Brigedia Jenerali Mabena,ametaja makambi hayo kuwa ni JKT Rwamkoma Mara, JKT Msange Tabora, JKT Ruvu Pwani, JKT Mpwapwa na Makutopora Dodoma, JKT Mafinga Iringa, JKT Mlale Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba Tanga, JKT Makuyuni Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa na JKT Mtabila Kigoma.
Makambi mengine ni JKT Itaka Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa Rukwa, JKT Nachingwea Lindi, JKT Kibiti Pwani na JKT Oljoro Arusha na kuongeza kuwa kwa wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho waripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi Pwani ambayo ina miondombinu ya kuwahudumia watu hao.
Hata hivyo Brigedia Jenerali Mabena,amesema kuwa wahitimu Wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho wametakiwa kuripoti katika kambi ya Ruvu JKT iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa Jamii hiyo.
Pia JKT limewataka vijana hao kuja na bukta ya rangi ya Dark blue yenye kiuno iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini isiyo na zipu na vingine ambavyo vimeanishwa.
Vingine ni track suit ya rangi ya kijana au bluu, nyaraka zote zinazohitajika katika usajili wa kujiunga na elimu ya juu, zikiwemo vyeti vya kuzaliwa na vyeti vya kuhitimu kidato cha nne.
Ameongeza kuwa “ Orodha kamili ya majina ya vijana hao Makambi ya JKT waliyopangiwa na maeneo ya makambi yalipo na vifaa wanavyotakiwa kuripoti navyo inapatikana katika tuvuti ya JKT ambayo ni www.jkt.go.tz
Mkuu wa JKT Meja Jenerali Rajabu Mabele anawakaribisha vijana wote waliohitimu kidato cha sita mwaka 2023 kuungana na vijana wenzao ili kujengewa uzalendo, umoja wa kitaifa, kufundishwa stadi za kazi, stadi za maisha na utayari wa kulijenga na kulitumikia Taifa” amesema.
Social Plugin