LISU ATAKA WALIOMSHAMBULIA KUSAKWA UPYA


Na Dotto Kwilasa, DODOMA.

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)Tundu Lissu amefika katika kituo kikuu cha Polisi Dodoma kuona gari alilokuwemo ndani yake wakati akishambuliwa September 7,2017 Jijini hapa eneo la Area D.


Akizungumza leo Mei 9,2023 na Waandishi wa habari kwenye eneo ambao gari hilo limeegeshwa amesema kwa mara ya kwanza tangu alipo shambuliwa ameliona gari lake kwani tangu ashambuliwe hakuwahi kuliona.

Aidha ameliomba Jeshi hilo kuendelea kumsaka aliye husika na shambulio dhidi yake na kumshughulikia kwa mujibu wa Sheria. 

"Nilifanya mawasiliano na uongozi wa Jeshi la Polisi Dodoma nashukuru wameniwezesha kuliona,nimehesabu matundu ya risasi yapo 30,imenifikirisha sana kwamba risasi zile zilielekezwa Kwa mtu mmoja ni unyama wa hali ya juu,"amesema

Ameongeza kuwa mara baada ya kukamilisha nyaraka muhimu atachukua gari hilo ili maisha mengine yaendelee.

Kuhusu maneno yaliyopo kwamba Polisi walizuia gari hilo Lissu amesema huo ni uvumi na kwamba hakuna siku amewahi kukatazwa na Jeshi hilo kuona gari lake.

"Kuchukua hii gari sio kwamba naondoa au nafuta kesi , kulingana na Sheria za Tanzania kesi za aina hii zinahesabika kama jinai,kesi hízi huwa mali ya Jamhuri,Mimi sina uwezo wa kuamua kesi ifanyike au isifanyike Mimi natumika kama shahidi tu,"amesisitiza

Mbali na hayo Mwanasiasa hiyo amekanusha tuhuma za  kukataa kutoa ushirikiano kwa Jeshi la Polisi kuhusu kushambuliwa kwake na kusema hajawahi kufanya hivyo kwani anaelewa hilo ni kosa la jinai na halikubaliki kisheria. 

"Puuzeni maneno ya kijingajinga ,siku zote Nimekuwa nikitoa ushirikiano kwa Polisi na hadi Sasa natamani huyo aliye nipiga risasi zote hizo atafutwe na ashughulikiwe kisheria,"amesema.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post