Wadau mbalimbali wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wanashiriki Maonesho ya Pili ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi (TVET) 2023, ambayo yanayofunguliwa rasmi hii leo na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.
Wadau hao vikiwemo Vyuo Vikuu, Bodi ya Biashara, Utalii na Mipango, Bodi ya Sayansi na Teknolojia, Mamlaka za Elimu, Wanafunzi wenye ulemavu wa akili, usonji, viziwi na uoni pamoja na Wajasiriamali wanashiriki maonesho hayo kwa kuonesha bidhaa wanazozalisha.
Maonesho hayo ya wiki moja yalianza rasmi Mei 16, 2023 na yatahitimishwa Mei 22, 2023 yakiwa na kauli mbiu inayosema Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi kwa Nguvu kazi Mahiri."
Social Plugin