MBUNGE wa Singida Mashariki Miraji Mtaturu amekabidhi kompyuta na printa kwa shule ya sekondari Mkiwa iliyopo wilayani Ikungi mkoani Singida.
Hatua hiyo ni kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan za kuboresha elimu na kuifanya Tanzania kuwa ya kidigitali.
Akikabidhi vifaa hivyo Mei 5,2023,Mh.Mtaturu amesema vifaa hivvyo vitasaidia kupunguza gharama za uchapaji na kudurufu nyaraka ikiwemo mitihani.
“Nimewakabidhi vifaa hivi kwa ajili ya matumizi ya shule,najua mnatumia gharama mkitaka kudurufu nyaraka na mitihani ya majaribio hapa shuleni,niwaombe mvitunze vifaa hivi na kuvitumia kwa lengo tarajiwa.
Machi 26,2023,Mh.Mtaturu alikabidhi kompyuta 5,printa na projecta kwa shule ya sekondari ya Issuna iliyopo wilayani Ikungi,Mkoani Singida.
Social Plugin