Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

POLISI SHINYANGA WAKAMATA HIACE MBILI



Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga limefanikiwa kukamata gari mbili aina ya Hiace zenye usajili namba T 202 BTW na T 358 DKM kwa kosa la kupakia nyaraka za serikali(vehicle inspection report) kitendo ambacho ni kinyume na sheria za nchi.


Akizungumza na waandishi wa habari leo Mei 26,2023 Kamanda wa Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga ACP Janeth Magomi amesema katika kipindi cha mwezi mmoja kuanzia tarehe 28/04/2023 hadi leo Jeshi la polisi limefanikiwa kufanya misako na operesheni mbali mbali kwa lengo la kuzuia na kukamata watuhumiwa waliofanya uhalifu.


Magomi amesema katika kipindi hicho Jeshi la polisi Mkoani humo limefanikiwa kukamata vitu mbalimbali ikiwa ni pamoja na Mirungi bando 24,Bhangi kete 206,Pikipiki 05,viti vya plastic 04,Vigae box 08,Battery za minara ya simu 02,Vifaa vya pikipiki,Mashine za kurandia mbao 02,Redio 03,Ng'ombe 13 zilizokiwa zimeibiwa,TV 08 aina tofauti tofauti,Baiskeli 02,Vifaa vya kupigia ramli,mbao 08,Msumeno 01,pampu ya maji 01,na Mabati 19,vipande vya chuma 07 vilivyokuwa vikitumiwa na wahalifu.


Aidha katika kuendeleza kudhibiti matukio hatarishi ambayo yanasababisha ajali za mara kwa mara Jeshi la polisi limeendeleza operesheni ya kukamata madereva waliokiuka sheria za usalama barabarani za makosa ya mwendokasi kwa kutumika VTS (vehicle tracking system).


"Jumla ya madereva 11 wa kampuni mbali mbali za mabasi ya kubeba abiria wamefikishwa mahakamani kwa kosa la kuendesha mwendokasi kati ya 90kph na 99kph na madereva 932 walikamatwa kwa kutumia speed ya radar na VTS wakiwa kwenye mwendokasi kati ya 80kph na 89pkh na kuandikiwa faini",amesema Magomi.


"Pia tumeweza kupunguza matukio ya ajali za pikipiki kwa kufanya operesheni ya kukamata makosa mbali mbali ya waendesha pikipiki na jumla ya pikipiki 1,417 zimekamatwa", ameongeza.


Vile vile Jeshi la polisi Mkoa wa Shinyanga linatoa wito kwa wananchi wake kufuatia sheria za nchi na kutojihusisha na vitendo vya kiuhalifu sambamba na kutoa onyo kwa madereva wote kutii na kuheshimu alama,michoro na sheria za barabarani wakati wanapokuwa barabarani na kwamba halitosita kumchukulia mtu au kikundi cha watu hatua za kisheria kwa yeyote atakae jihusisha na vitendo vya uhalifu.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com