SERIKALI KUGHARAMIA MATIBABU YA MAJERUHI WA AJALI YA ROLI BAHI


Na Dotto Kwilasa, Dodoma.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma amepiga marufuku magari ya mizigo kutumika kubeba abiria katika mkoa huu ili kunguza ajali zinazosababisha vifo ambavyo vinaweza kuzuilika.

Hatua hiyo ni kufuatia ajali iliyoua wanafunzi wawili jana Mei 11,2023 wa shule ya Sekondari ya Mpalanga wilayani Bahi mkoani hapa kupoteza maisha kwenye ajali ya lori la mizigo lenye namba T519 DSY, lililotumika kubeba abiria.

Mkuu huyo wa Mkoa wa Dodoma ameongea hayo wakati  akizungumza na wakazi wa wilaya ya bahi mara baada ya kutembelea familia za wafiwa na  kuwapa pole majeruhi ambapo ameeleza kuwa Serikali itagharamia matibabu ya majeruhi pamoja na mazishi ya waliofariki kwenye  ajali hiyo.

"Acheni kuishi kwa mazoea hasa katika matumizi ya vyombo vya usafiri ili kupunguza athari inapotokea ajali,nawaomba wafiwa kuwa na moyo wa subira katika kipindi hiki kigumu kwenu,

na nitakuwa bega Kwa bega na Jeshi la Polisi kuhakikisha wahusika wa ajali wanachukuliwa hatua za haraka;

Naye Mkuu wa Usalama Barabani wilaya ya Bahi, ASP Bakari Ramadhani amesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa gari hilo lililobeba wanafunzi ambao ulisababisha gari kumshinda dereva na kuacha njia Kisha kupindua.

Amesema Kutokana na ajali hiyo  Jeshi la Polisi linamshiria Dereva huyo kwa hatua zingine za kisheria.

Naye, Yohana Bebeyo  baba wa marehemu Neema Hoya aliyekuwa mwanafunzi wa kidato cha pili, alisema amepokea taarifa za msiba huo kwa masikitiko makubwa.

“Mwanangu alirudi kutoka kambini siku moja kabla ya siku ya tukio, kuhitaji hela ya matumizi na leo asubuhi ameondoka baada ya muda tunapokea taarifa kuwa amekufa inasikitisha sana”amesema

Ikumbukwe kuwa katika ajali hiyo wanafunzi wawili wa kike wamefariki dunia papo hapo majina yao ni Neema Yohana Hoya (17) kidato cha tatu mkazi wa Chidilo na Magreth Juma (19)  mkazi wa Nholi na wanafunzi 31 walipelekwa hospitali ya Rufaani Dodoma kwa matibabu na wengine 14 walipatiwa matibabu zahati ya Mpalanga.

Aidha kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na kitengo cha mawasiliano serikalini inafafanua kuwa gari hiyo yenye namba za usajili T 519 BSY aina ya Mitsubishi Canter ilibeba wanafunzi 51, Walimu wawili kutoka Mpalanga Sekondari, wakielekea shule ya Sekondari Magaga kushiriki michezo ya UMISETA.


Hata hivyo, mwili wa Neema Hoya ulitarajiwa kuzikwa jana huku mwili wa Magrth Shimba, ukisafirishwa kuelekea Kishapu mkoani Shinyanga kwa ajili ya mazishi.



Mwishoo

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post